Kwa iyo mkuu, maneno yote haya, main point yako, ni bora Magu asingelifufua shirika la ndege la taifa.Najiuliza hivi kuna siku imewahi kutokea watu wakabaki pale air port kwa kukosa usafiri wa Kwenda Marekani au Dubai kwa kukosa usafiri?
Bil. 500 kununua ndege sio jambo dogo lakini kwa mazingira na matatizo tuliyonayo hiyo sio biashara nzuri kwa serikali.
Hiyo nayo ikichunguzwa vizuri ni janga la baadae na hasara.
Kwa nini tunashindwa kuwatumia matajiri wa ndani kufanya biashara hizo kwa ubia na serikali au hata kwa wao wenyewe?
Watoto wengi wa maskini wamekosa mikopo vyuoni. Hizo pesa wangekopeshwa hata kwa riba ingekua ni jambo ukombozi mkubwa kwa taifa letu kuliko kununua ndege .
Kuwasomesha watoto wa mama Tanzania ni faida kubwa kuliko kununua ndege.
Hizi biashara ni za muda mfupi sana ndio maana Wenzetu wa nchi Tajiri wanawapa fursa zaidi wawekezaji kwenye biashara mana serikali kufanya biashara ni jambo gumu sana.
Hebu fikiri 2025 Mh.Magufuli atakapostaafu na mtoto wa waziri au katibu fulani au mkuu fulani wa mkoa au kada wa CCM na mtoto wa mkulima wote wamemaliza chuo cha urubani na waombe nafasi za urubani ; je , ni yupi atakayepata ajira kati ya hao wawili yaani mtoto wa mkulima na mtoto wa waziri?
Ikumbukwe kuwa hizi sio sera za taifa za uchumi bali ni maona na sera za chama.Ikiwa na maana ya wazi kuwa zina upinzani na kukosolewa kuanzia ndani ya chama. Hivyo ni wazi kuwa zitaungwa mkono kinafiki kipindi hiki cha awamu hii ambayo kwa kiasi fulani ina kiongozi mwenye msimamo Mkali.
Bil. 500 zingewekezwa hata kwenye mafunzo ya JKT na kuwa kama vyuo vya ufundi badala ya kutumia muda mwingi kwa mafunzo ya kijeshi kwa watu wasio wanajeshi ingekua ni jambo bora sana kwa ajili ya kuandaa Tanzania ya Viwanda.
Watalii kuja Tanzania au watu kusafiri kwenda nje ya nchi wana njia mbadala za usafiri na wanazitumia siku zote lakini watoto wa maskini hawana mbadala pale wanapokosa elimu kwa kukosa mikopo.
Kuwa na watalii wengi pia inategemea na diplomasia yetu imejipanga vipi. !!
Nchi yetu imewahi kutembelewa na Papa mara kadhaa na marais wa Nchi kubwa duniani pamoja na kuwa hatukuwa na ndege lakini diplomasia yetu ilifanikiwa hayo yote. Hata uchumi wetu wa utategemea diplomasia yetu.
Pia ushindani wa kibiashara nayo itakua ni kikwazo kikubwa sana. Yapo mashirika Makubwa sana ya ndege yenye ndege nyingi sana ambayo yanategemea faida kidogo kujiendesha kutokana na ukweli kuwa yapo kwenye biashara kwa muda mrefu. Na biashara kubwa mpya zenye ushindani mara nyingine zinahitaji matangazo kwa gharama kubwa sana. Ni moja ya kuongeza gharama za uendeshaji.
Je, ATCL wana nia ya dhati au wanalinda ajira zao tu kwa kushawishi ununuzi wa ndege kwa pesa za kodi ya watanzania mbali na pesa zao zinazotokana na faida waliyopata tangu kuanzishwa kwa shirika hilo?
Je,kwa nini siku zote walishindwa kununua hata bajaji leo hii wanaibuka na kuomba wanunuliwe ndege mpya?
Hayo tuwaachie wataalam na wanasiasa waliowaza kufanya biashara hiyo kwani wote tungependa kuona mafanikio na sio hasara. Tunapenda tuone nchi yetu ikisonga mbele kwa kasi na ATCL wanafanya vizuri bila kurudia makosa .
Atasaidiwa kuiba riziki aka ruzuku mkuu!na bajeti ya lipumba ni kiasi gani ili aue CUF