Aina za wanaume waoaji

Aina za wanaume waoaji

Yes Yes Yo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2014
Posts
232
Reaction score
99
Kuna Aina Kadhaa Za Wanaume Waoaji Ambazo Biblia Imezitaja Ambazo Ni Zilezile Ambazo Tunazo Hata Sasa Kwenye Kizazi Chetu:

1.WANAUME AMBAO "YEYOTE ALIYECHAGULIWA NA KUKUBALIWA NA WAZAZI" BASI YEYE ANAMPOKEA TU... [ISAKA NA REBEKA]!

Hii Ni Aina Ya Wanaume Ambao HAWATAKI KUWACHUKIZA WAZAZI WAO, Na Wako Tayari KUUFANYIA KAZI USHAURI WA WAZAZI KWENYE SWALA LA MKE YUPI WAOE (CHAGUO LA WAZAZI).
Isaka Alipofikia Muda Wa Kuoa, "HAKUJICHAGULIA MKE" Bali Baba Yake Mzee Ibrahimu Alihakikisha ANAMTAFUTIA MKE Kupitia MFANYAKAZI WAKE MMOJA MWAMINIFU ALIYEKUWA AMEMWAPISHA KWA BWANA Kwamba ATAMLETEA MWANAE Binti ASIYETOKA MIONGONI MWA BINTI ZA KANAANI!
Katika Hili Kundi, KUNA AINA MBILI ZA WAZAZI PIA:

-Wazazi Wanaomwendea Mungu Kumuuliza Kuhusu Mke Sahihi Kwa Kijana Wao.... Ibrahimu Na Yule Mtumwa Wake Aliyemtuma Kumtafuta Mke WALIMSHIRIKISHA MUNGU Kumpata Mke Sahihi Kwa Ajili Ya Isaka.
NI MARA MIA KUWA NA WAZAZI "WACHA MUNGU" Ambao HAWATACHAGUA MKE/ MME WA MTOTO "KWA AKILI ZAO BALI KWA MSAADA WA MUNGU ANAYEJUA YOTE"

-Wazazi Ambao Hawamuulizi Mungu Kuhusu Mke/ Mme Sahihi Kwa Mtoto Wao Bali WANATUMIA VIGEZO VYA KIBINADAMU Kama Vile KABILA LAKE, HALI YAKE YA UCHUMI, KIWANGO CHA ELIMU, FAMILIA ANAYOTOKA Nakadhalika.
Hawa Ni WAZAZI BOMU Ambao WANACHAGUA MWENZI KWA MTOTO Ilihali ATAKAYEISHI NA MKE/ MME Ni KIJANA WAO NA SI WAO Ingawa Wao Ndio Wanaweka VIGEZO NA MASHARTI!

2.WANAUME WANAOPENDA KUOA WANAWAKE "MABIKIRA" NA WASIOWAJUA "WANAUME"...

Kwenye Biblia Wako Wanaume Kadhaa Ambao Wao WALIKUWA WANAOA KWA KUANGALIA KIGEZO CHA "UBIKIRA" WA MWANAMKE, Baadhi Yao Ni MFALME AUHUSUERO Aliyemwoa MALKIA ESTA Aliyekuwa Bikira, YUSUFU [Baba Mlezi Wa BWANA YESU] Huyu Alikuwa Amemposa BIKIRA MARIAMU [Mama Mzazi Wa Yesu] Na Alipogundua Mariamu Ni MJAMZITO, Biblia Inasema ALIAMUA "KUMTOSA KIMYAKIMYA" Mpaka Pale MALAIKA WA BWANA ALIPOMTOKEA KWENYE NDOTO NA KUMWAMBIA "HUYU BINTI HAJAKUSALITI, HII MIMBA NI KWA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU" Ndipo Aliporudi Na Kumchukua Tena Mariamu!

Ziko Aina Mbili Za Wanaume Wa Aina hii:

-Wale Ambao NAO WAMEJITUNZA [HAWACHEZI MPAKA NDOA] Na Wamemwamini Mungu Kuwapa WATU WALIOJITUNZA KAMA WAO

-Wale Ambao HAWAJITUNZI [NI WAHARIBIFU NA WACHAFU] Wao WANARUKARUKA TU Lakini WANAPENDA WAPATE "WASICHANA MABIKIRA"
Hawa Mimi Nawaita "WASHENZI WA TABIA"

3.WANAUME AMBAO WAKO TAYARI KUOA "MWANAMKE YEYOTE ILIMRADI MUNGU AMESEMA WAOE HUYO" BILA KUJALI HISTORIA YAKE YA NYUMA...

Kwenye Biblia Yangu Kuna Watu Kama NABII HOSEA Ambaye Mungu Alimwambia AKAMTWAE NA KUMWOA MKE WA UZINZI [MWANAMKE KAHABA] Na Yeye Bila Kusita Au Kujiuliza Mara Mbili AKATII SAUTI YA MUNGU NA KUOA MWANAMKE "ANAYEJIUZA" Sawasawa Na MAAGIZO YA MUNGU
Hawa Ni Wanaume Ambao "WANAMJUA MUNGU WAO KWELIKWELI" Na Wanajua KUITAFSIRI SAUTI YA MUNGU NA KUITII.
Wako Wengi Ambao Mungu Amewahi Kuwaambia WAOE WAKE/ WAOLEWE NA WAUME FULANI Lakini WAKAKATAA Na Kuolewa KWA VIGEZO NA MASHARTI "WALIYOJIWEKEA" Lakini Hadi Leo NDOA ZAO ZINAYUMBA NA ZINA MSHKELI USIOKUWA WA KAWAIDA!
Mungu ANaweza Kumwambia MSOMI MKUBWA AOE/ AOLEWE NA MTU ASIYE NA ELIMU KUBWA AU AMBAYE HAJASOMA.... Anaweza Kumwambia KIJANA TAJIRI AOE/AOLEWE NA KIJANA MASIKINI AU HATA MJANE FULANI ALIYEFIWA NA MME HII KARIBUNI... Lakini UTIIFU AU KIBURI CHA MHUSIKA NDICHO KINAAMUA!

4.WANAUME "WAKOMAVU KATIKA UPENDO NA IMANI" WENYE MOYO NA MTAZAMO KAMA WA BWANA YESU; HAWA WANAAMINI KWENYE NGUVU YA UPENDO NA IMANI KUMGEUZA MTU... MAADAMU MUNGU AMEWAPA "GO AHEAD" YA KUOA MTU FULANI... HAWAANGALII HALI YAKE YA SASA WALA BACKGROUND YAKE, BALI WANAANGALIA "POTENTIAL ALIZONAZO" AMBAZO ZIKIUNGANA NA "NEEMA YA MUNGU, UPENDO NA IMANI" ZINAWEZA KUMFANYA HUYU MWANAMKE MTU BORA....

Kwenye Biblia Kuna Mfano Wa "MWANAMKE MSAMARIA" Ambaye BWANA YESU Alipomwendea ALIJUA WAZI KWAMBA "HISTORIA YAKE ILIYOPITA NA ILIYOPO NI MBAYA" Maana ALIKUWA AMEACHANA NA WANAUME WATANO NA HUYO WA SITA ALIYEKUWA NAYE "HAKUWA MME WAKE" BALI "BUZI TU"
Lakini YESU ALIJUA "HUYU MWANAMKE ANA POTENTIAL KUBWA SANA NDANI YAKE" Ambayo INAWEZA KUMFANYA BORA SANA "KESHO" Hivyo "KWA IMANI NA UPENDO" Akamtii MUNGU Na KUKAA KISIMANI AKIMSUBIRI Na Alipofika AKAMWONESHA UPENDO WA MUNGU NA IMANI; KWA NEEMA YA MUNGU AKAGEUZWA NA KUWA "MTU MPYA" Na Saa Ilieile Akaondoka KURUDI MJINI Na Kuanza KUCHAPA INJILI NA KUULETA MJI MZIMA WA SAMARIA "KWA YESU" Kule Kisimani!
YESU HAKUANGALIA MAPUNGUFU YA MWANAMKE HUYU Bali Aliangalia POTENTILA YAKE Na KWA UPENDO, IMANI NA NEEMA "AKAMVUTA KWAKE" Na Mara Yule Mwanamke Msamaria Akawa Bora Na KUPIGA INJILI NA KUULETA MJI MZIMA WA SAMARIA KWA YESU!

Wako Wanaume Wa Aina Hii Na Wanawake Wa Aina Hii; Ambao Wao HAWAANGALII MAPUNGUFU NA MATATIZO YA WENZI WAO Bali Wanaziangalia POTENTIAL WALIZONAZO Ambazo ZIKILELEWA, KUKUZWA NA KUENDELEZWA Kwa UPENDO Kwa UONGOZI NA MSAADA WA ROHO MTAKATIFU Zinawafanya Wenzi Wao Kuwa WATU BORA KWA BWANA, KANISA NA HATA TAIFA NA DUNIA YAO.
 
Huyo wa tatu do hasa anayehitajika katika kizazi cha sasa ambacho kuipata bikira ni kwa tochi,huwa nawashangaa wanaume wanaosujudia bikira karne hii ambayo kimsingi haileti maendeleo inaleta heshima kwa mume tu,saizi ni kufikiria mwanamke ambaye anapotential mnaweza kusaidiana katika maisha hapa simaanishi awe na kazi sijui elimu hizo ni mbwembwe tu tumeona wasomi wangapi ndoa zinawashinda hapa anatakiwa mwanamke ambaye anajitambua na anajua wajibu wake katika ndoa kama mwanamke anayependa maendeleo kama Yesu alivyo angalia potential kwa msamria,hapa najiuliza kama toka enzi za Yesu walikuwepo wanawake wanaoweza kuwa nawanaume sita leo hii mwanaume atafute bikira kweli mmmh! hizo bikira mnawatoa wenyewe halafu mnawaacha halafu wakati wa kuoa mnataka bikira wale mliowatoa na kuwaacha awaoe nani?
 
Ahsante sana kwa mada nzuri. Leo nimekutana na mafunzo bora kabisa. Hii ni miongoni mwa sauti ya mtu anayeita mtandaoni.
Mimi nipo namba 4. Wasichana msinione mbaya, kwa sasa acha iwe hivyo.
 
Ahsante sana kwa mada nzuri. Leo nimekutana na mafunzo bora kabisa. Hii ni miongoni mwa sauti ya mtu anayeita mtandaoni.
Mimi nipo namba 4. Wasichana msinione mbaya, kwa sasa acha iwe hivyo. Je nitapata msichana wa kufanana naye. Mungu saidia.
 
Hvi unamjuaje kwamba hyuy ndiye uliechaguliwa na Mungu?
 
Back
Top Bottom