Aina za Uchawi wa Kisambaa

Aina za Uchawi wa Kisambaa

jf nimejiunga 9/9/2014 kuna mambo meng hupaswi kumjudge mtu kutokana na info unazozijua kwake
 
uchawi haupo
Yaliyonikuta huko usambaani sina hamu nao!!ki ukweli huo uchawi wao kama wakiuweka wazi wangekuwa mbali sana!!kulikuwa na kazi tunafanya huko,kwa kutumia generator,tukawa tumezungushia warning tape ili mtu asiyehusika asiingie humo!!mala akaja mzee mmoja akaingia humo,tukaenda kumtoa aka mind kishenzi!!tukafunga jioni tukaenda kulala kwenye nyumba tuliyokuwa tumepanga,bnana asubuhi wote sita tumeamka miili inauma halafu kwenye mabega tuna yale malanda ya mbao na mikwaruzo kwaruzo heeee,tukaenda kwa mwenyeji wetu kumuelezea alicheka sana!!!akasema nyie nendeni tu kazini,nitakuja huko huko!!tumefika site washa jenerata wapi,tukamtafuta fundi,akaja akalikagua haoni tatizo lolote,akajiongeza alasema hebu tulitoe hapo site twende nalo center kama km tano,kutoka site!!akasema hebu washa sasa,kick moja tu likawaka akacheka sana!!!kila ukizima unawasha tu,haya turudi site,tumefika washa na wewe wapi!!fundi akaondoka akasema hili liko nje ya uwezo wangu!!!ndipo akaja yule mwenyeji wetu tukamueleza ,akasema powa ngoja niende home kuna kitu nikachukue,akasema yule mzee ndio zake hizo lakini leo,nitapambana naye,akachukua kibuyu na dawa dawa,fulani,akaongeaa maneno na kuzichoma,badaye akasema hebu washa!!BNANA kick moja tu jenerata hiyooooo!!!daaa haya mambo,hadi tunamaliza kazi ile zaidi ya wiki mbili hatukupata shida yoyote ile!!!ila alituonya tu ni marufuku kulia nje kitu chochote kile.
 
ushinga na ntigo si zina maaana sawa
Ushinga huponi, ukitegewa hauchukui masaa ya kuwepo duniani, ila inategemeana na aina ya ushinga

Nimeshawahi kuwaona waliotegewa na kuwazika, wanakufa kifo cha mateso tumbo na kiuno vinauma sana, mwisho akishakata kauli mlingoti unasimama, na huzikwa ukiwa dede
 
Mungu ni mwema

twende moja kwa moja kwenye Mada naomba tu nsieleweke vibaya mimi sio mchawi mganga au mtaalamu sana wa mambo hayo lakini kuna namna naweza kuwasaidia watu kutokana na aina hizi za uchawi ninaoujua kutoka kwenye jamii za wasambaa sehemu nilipokulia kusomea kuolea na hata kujenga huko ijapokua mimi kwa asili ni mchaga Mmarangu wa Old Moshi

KIATU
huu ni aina ya uchawi wanaotumia wachawi wa kisambaa ambao lengo kuu l mchawi ni kumpeleka mbali sana mtualiyekusudia kumroga yaani ukipigwa kiatu unatembea tu kila siku unaenda mbali na kwako au kwenu hukumbuki nyuma wala utakua huna mpango wa kurudi nyumbani

NTIGO
sijui kama nimesound vizuri aina hii ya uchawi ipo kwa lengo la kuwalinda wake au watoto wa kike ukitembea na mke wa mtu unaweza kuumwa kuanzia kwenye kiuno kushuka chini hapa ieleweke sio lazima mume wa huyo mke awe amekuonya au sio lazima uwe unajua kuwa ni mke wa mtu yaani kutembea naye tu unaumwa kupona kwa huo ugonjwa ni lazma umtafte mume wa mke uliyetembea naye mbagain umpe ngombe au fedha ufanyiwe uganga upone

MVUAZA

Huu ni aina ya uchawi ambao mhusika anaununua rasmi kwa ajili ya kuogopeka au kukwepa madeni ukiwa na mvuaza unaweza kuwa unadaiwa lakini ukikutana na mtu anayekudai ile nguvu aliyokua nayo ya kudai inapungua anacheka cheka au anakusamehe kabisa
pia kama una case mvuaza humfanya aliyekushitaki asahau kwenda mahakamani au afute kesi au faili la case lisionekane

ZONGO
Hii ni aina ya uchawi ambayo lengo kuu la mchawi ni kupima kinga zako za kichawi zongo humfanya mtu aumwe ghafla atapike au tumbo livurugike mara nyingi zongo hutumwa kipindi unakula kitu chochote mbele ya mchawi zongo hutumwa kwa njia ya kujikuna kuna ukiona unakula alafu mtu anajikuna kuna mbele yako mkanye mwambie tu acha ujinga wako ataacha na atajua ww ni mtaalamu wakati huna utaaalamu wowote
Zongo baya ni la kulogwa ukiwa unakula msibani uuguzi wake ni lazima upate chakula kingine cha msibani ndio uaguliwe nao

KOPERA
huu ni uchawi wa kuibiana vitu kwa njia ya mazingara unaweza kuibiwa Mazao pesa au hata akili kwa wale mnaosoma yaani ni uwezo anaokua nao mchawi wa kuhamisha mali yeyte anayoitaka kuna njia nyingi za kukabiliana na hali hiyo lakini zinazojulikana ni kuweka mfupa wa nguruwe kumwaga/kuweka chumvi ya mawe /kutumia ndulele 2/3 kwenye mali yako pia maombi kwa wale tunaomwamni Mungu
UPDATES
SHAKIIZI

huu ni aina ya uchawi ambao mchawi hutuma jini kwa mtu aliyekusudia ili ajidhuru au adhuru wengine
mhusika anaweza kuua au kugombana na ndugu zake bila kujitambua Shakiizi huweza kusababisha mtu kufanya jambo bila kukusudia na akishalifanya hujutia sana


kama kuna ulilowahi kukutana nalo au unajua uchawi mwngine tuelezeane
Umesahau USHINGA

Ukila mke wa mtu wanakuonya kama husikii unaendelea kumla huyo mwanamke

Basi watamwekea mwanamke USHINGA siku ukiingiza tu libolo FC hapa sehemu ya chini ya mwili wako inakufa ghafla na unaweza kufa Moja kwa moja.

Pona Yako wakikuwahisha kwa wataalanu

Utakatwa miguu utakuwa kilema maisha Yako yote.

Nimeshwa shuhudia mtu akiwa mzima tu one day nakutana nae Hana miguu anajiburaza mtaani na mikono ndio kuuliza ilikuaje yule jamaa wakaniambia USHINGA mzee huo

Wasambaa nuksi sana
 
Haya mambo yapo ila watu wanaangamia kwa kukosa maarifa, hasa kwa kuzingatia hizi dini za kigeni. Ukipigwa na huo uchawi ukiendekeza kusali unapoteza maisha.
umeandika jambo la maana sana ushukuriwe hapa nipo napambana na uchawi wa wazazi wangu wamenipa vipele vya joto nikikaa kwa jua mwili unasikia kama unachoma chomwa na sindano nyingi hadi unavimba aisee watalipanaskia unaitwa CHAWA NI UGONJWA MPYA.

Haya mambo yapo ila watu wanaangamia kwa kukosa maarifa, hasa kwa kuzingatia hizi dini za kigeni. Ukipigwa na huo uchawi ukiendekeza kusali unapoteza maisha.
 
Back
Top Bottom