11. NDOA YA VITISHO.
Hii mwanamke huolewa kwa vitisho vya kilaghai.
Jamaa hutumia njia za hila baada ya kuona mwanamke anasimamia 'sitaki' yake.
Huanza kutoa vitisho kwamba 'tutaona', hapo maana yake kuroga na kuigiza kama kweli kadhamiria kuua mtu kwa ndumba.
Ama mwanamke kuburuzwa kwenye vyombo vya sheria kukandamizwa kutokana na maneno yake ya kejeli ama kiburi aliyoyatoa akipinga kuolewa huko.
Mwisho wa siku mwanamke hulegeza masharti na jamaa kuokota dodo kwa tabu.
Ndoa hizi hudumu kwa sababu jamaa humlea mwanamke kama yai, kwa kuwa alimpata kwa kugaragazwa na kudhalilishwa mno, hawezi kuchezea shilingi chooni.
Kubembelezwa na kudekezwa kote huko, saazingine mimba za dabodabo huwekwa sawa, mwishowe mwanamke hujishitukia kapenda kidhati juu kwa juu na kudumu kwenye ndoa mazima.