Aina Mpya ya Ufisadi nchini Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aina Mpya ya Ufisadi nchini Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by STEIN, Jun 28, 2011.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Peoples Power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Nimegundua aina mpya ya ufisadi hapa nchini kwetu na hasa hii inawaathiri Vijana wasomi. Ufisadi huu ni ule wa makampuni mengi makubwa na madogo kuwaajiri ndugu zao ambao si watanzani, hasa wahindi , waarabu, wazungu, wkenya kwa kisingizio cha hawa ni watalamu ile hali watanzania wakiachwa bila kazi na wengine kuachishwa kazi bila sababu za msingi. Nina mifano ya makampuni hayo na nikihitajika nitayataja na wafanyakazi wanaowaita experts wakati kimsingi wanafahamu kiingereza tu. Ukija kwenye uwezo wao wa shule na uzoefu utakuta hawana lolote.

  Nina jina la kampuni ambayo walimchukua mhindi kutoka india na wakampa Mtz, kazi ya kumtrain baada ya mhindi kuelewa kazi wakamwachisha MTz na sasa yuko mtaani, kwa yeyote anayehitaji ushahidi niko tayari kuutoa hata mahakamani.

  Kuna makampuni kibao wageni wanafanya kazi hata bila kuwa na kibali na wanalipwa mshahara wa kati ya dola 5000 na 25000 huku wengine wakiwa hawana hata vibali kutoka uhamiaji. Hivi watanzania wanakosa kazi huku wageni wakijazana humu nchini kwa nini? Hivi idara uhamiaji inafanya nini au wanasubiri hadi vijana tuanze kuchukua sheria mkononi ndio waje watupige mabomu ya machozi?

  Makampuni mengi siku hizi yanafanya kazi ya kutangaza nafasi za ajira lakini kiuhalisia hakuna anayeajiriwa, mfano upo wanatangaza kazi kila gazeti lakini sioni anayechukuliwa wa.

  Kama hii hali haitarkebishwa, vijana wote tuwe pamoja na kuhakikisha kuwa hali hii inatokomezwe, najua hili bomu litalipuka muda wowote, ukija kwenye biashara wachina wamejaa kila kona wanatoa vitu kutoka kwao wanakuja kuuza humu kwa bei ya jumla reja reja watanzania tutatokaje. Nadhani hili halina ubishi uwe CCM, CUF wala CDM wote tunapigika maana nachoshukuru ni kwamba CDM wamebana kiasi kwamba hakuna tofauti kati ya kada wa CCM na CDM wote tuna pigika.

  Swali langu la mwisho kwa watanzania wanaofanya kazi nje, je na wao wanafanya kazi bila Permit? Je kodi hawakatwi?

  Hii ni aina mpya ya ufisadi utadhani ni shama la bibi, kila mtu avune anachokitaka. Hii haiwezekani au Vijana mnasemaje? Nchi ishauzwa tuikomboe.
   
 2. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Duh! hii yaweza kuwa kweli, ila twaomba mifano halisi.
   
 3. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  this has been there for quite some years. hii ndo faida ya rais wetu kuwa ombaomba hajui kuwa hupewi kitu bure dunia hii sasa watu wao wamezagaa tz kama kwao, wengine huuza ndala na k.
   
 4. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  huu ni ukweli mtupu kama huamini nenda kwenye makampuni yote makubwa unayo fahamu utakuta ngozi nyeupu tu 40% the rest ndio weusi sasa najiuliza hivi watanzania wakuwa 40% weupe au ndiyo haya tunayosema?
   
 5. j

  jategi Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kuna tatizo kubwa kwetu sie watanzania hasa wenzetu waliofanikiwa kuanzisha makampuni na hata wananchi wa kawaida. Tatizo lenyewe ni kutothamini vyetu, yaani watu wetu, mali zetu na mazingira yetu, hiyo ndo sababu kubwa inayofanya makampuni yaajiri wageni na kuaacha watanzania maan wanadhani kwamba wageni hao ni bora kuliko watanzania. kama nilivyogusia kwenye sentensi yangu ya hawali, tatizo la kutothamini vyetu haliko kwa wenye makampuni tu, lipo hata kwetu watu wa kawaida na ukitaka kuthibitisha hilo, tembelea maduka na supermarkets, watanzania hatupendi kunua bidhaa zetu ila tuna nunua sana bidhaa za nje, tembelea hata bar zetu alafu mwombe muudumu wine iliyotengenezwa dodoma, ambayo kwa mtazamo wangu ni bora kuliko iliyotenegenezwa Afrika ya kusini, atakwambia hawana wine yoyote iliyotengenezwa Tanzaia bali wanazo zilizotengenezwa nchi zingine hasa Afrika kusini. Hali ya kutothani vyetu imekwenda mbali sana ndugu zangu mpaka kwenye mazingira yetu, ndo naana utakuta mtu anakunywa maji ya chupa akiwa kwenye daladala au gari lake binafsi na akimaliza anatupa chupa hovyo na mitaani kwetu tunatupa taka hovyo kana kwamba sie hatuishi maeneo hayo. Tujenge utamaduni wa kudhamini vitu na watu wetu na tutafanikiwa
   
Loading...