Aina mbalimbali za wenye nyumba

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,538
15,175
1: Wenyenyumba wastaafu au ambao hawaaendi popote muda wote wako nyumbani wanawafuatilia wapangaji utadhani mgamo wa jiji.
Hapa inabidi uwe na Moyo wa chuma, inginevyo utahama tu.

2: Wale ambao wanaishi mbali ila wakija hapo ni kivumbi, kelele, kugomba, kukosoa na kutisha.

3:Wale ambao wanawaonea wivu wapangaji wao, wakiona wanamaisha bora, wanakula vizuri wanafikilia kuwapandishia bei ya pango na kuwavuna zaidi.

4:Kuna wale washua wanapesa lkn wakikupa muda, ukipitiliza kulipa kodi ni kesi hata mahakamani utapelekwa hawataki longolongo. Hapa pia wapo washua ambao hawana uswahili wao wakiisha kukupangisha hawakufuatilii wanachotaka ulipe tu pesa yao.

5:Kuna wale wanaomvizia mke wako, au watoto wako wa kike ili wachepuke nao. Hawa nao wanaleta ukaribu na wanawake zaidi.Utawasikia '' Shemeji leo nikuote dina" hahaha

6:Kuna wale ambao wake zao wananguvu na wanawatawala, Hapo mkuu utake usitake huyo mwanamke ndiye atakaehamua ubaki au uondoke bila kujali umewakosea au la.

Vipi wakuu,
Umewahi kukutana na wenye nyumba wenye utata gani na uliwadhibiti vipi?
Wasaidie wapangaji wapya jinsi ya kupammbana na songombingo za wenye nyumba
 
Nimekutana na wenye nyumba wenye tabia zote ulizozitaja na ambazo hujazitaja. Maisha haya!
 
Na ambao bado tumepanga je?
ukipanga uswahilini utaelewa vizuri.
wengine tunawekewa hadi idadi ya wageni, ukitoka toilet lazima landlord aingie akague kama anaweza kupata kajambo kakukusimangia. hawa ni wale wazee ambao huwa nawana kazi wala mradi zaidi ya wapngaji.
 
Nimekutana na wenye nyumba wenye tabia zote ulizozitaja na ambazo hujazitaja. Maisha haya!
kweli mkuu maisha tu.
ukiwa na roho ndogo kila kodi ikiisha unahama.
kuna mmoja yeye wakija wageni wa mpangaji ananuna, ukibaki peke yako amani tele.
 
1: Wenyenyumba wastaafu au ambao hawaaendi popote muda wote wako nyumbani wanawafuatilia wapangaji utadhani mgamo wa jiji.
Hapa inabidi uwe na Moyo wa chuma, inginevyo utahama tu.

2: Wale ambao wanaishi mbali ila wakija hapo ni kivumbi, kelele, kugomba, kukosoa na kutisha.

3:Wale ambao wanawaonea wivu wapangaji wao, wakiona wanamaisha bora, wanakula vizuri wanafikilia kuwapandishia bei ya pango na kuwavuna zaidi.

4:Kuna wale washua wanapesa lkn wakikupa muda, ukipitiliza kulipa kodi ni kesi hata mahakamani utapelekwa hawataki longolongo. Hapa pia wapo washua ambao hawana uswahili wao wakiisha kukupangisha hawakufuatilii wanachotaka ulipe tu pesa yao.

5:Kuna wale wanaomvizia mke wako, au watoto wako wa kike ili wachepuke nao. Hawa nao wanaleta ukaribu na wanawake zaidi.Utawasikia '' Shemeji leo nikuote dina" hahaha

6:Kuna wale ambao wake zao wananguvu na wanawatawala, Hapo mkuu utake usitake huyo mwanamke ndiye atakaehamua ubaki au uondoke bila kujali umewakosea au la.

Vipi wakuu,
Umewahi kukutana na wenye nyumba wenye utata gani na uliwadhibiti vipi?
Wasaidie wapangaji wapya jinsi ya kupammbana na songombingo za wenye nyumba
Hutaki kusumbuliwa mbona simple jenga nyumba yako..
 
Wenye nyumba wana nguvu sana hasa mijini.Ila hakuna mwenye afadhali wote wana matatizo yanayokaribiana.
 
Back
Top Bottom