MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,264
Akiwahutubia Maelfu ya wakazi wa jimbo la Iringa mjini katika uwanja wa Mwembetogwa , Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alianza hotuba yake kwa kusema, " Nawaambieni wala hamta nisikia nikishughulika na kumzungumzia mbunge wenu hapa sina Time, mimi nashughulika na mambo ya wananchi kwani mbunge wenu ni kazi yake kutukana kila mmoja na kuhamasisha maandamano yasiyo kwisha "
Akihutubia huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi uwanjani hapo, Kinana alisema kuwa amefika jimbo la Iringa mjini kuwaeleza mambo ya kimaendeleo sio kumsema mchungaji Msigwa.
Aliendelea kusema, ''Napenda niwaambie kuwa, kazi zilizofanywa na CCM na serikali yake ni kubwa na kuwa hata miradi ya barabara inayoendelea kujengwa ni jitihada za serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete hivyo mbunge wenu hana sababu ya kujisifu kwa kazi hizo''.
Katibu mkuu huyo alieleza kusikitishwa kwake na ushuru mbali mbali kwa wananchi wanaojitafutia maisha yao huku viongozi wakijiweka mbinguni na wananchi wao. amewaahidi kukifikisha kilio chao kwenye Kamati Kuu ya CCM na serikalini.
Alisema kuwa ndani ya serikali hii mwananchi anatafuta haki yake hapati hadi atoe rushwa huku viongozi waliopo ndani ya CCM badala ya kushughulika na mambo ya wananchi wanashughulika na mambo yao wenyewe huku wakiendekeza ugomvi usio na mwisho .
" Tunapoteza majimbo na kata kwa ajili ya uroho wa uongozi kwa baadhi yetu na kushindwa kushuka kuwasikiliza wananchi wa chini hali inayozalisha malalamiko ya wananchi na kupelekea kuhamia vyama vya upinzania"
"Ni lazima kujiimarisha kuanzia ngazi ya chini kabisa ili kupata ushindi ikiwa ni pamoja na kuondokana na makundi ambayo yanakigawa chama,"anasema.
Hivyo alisema kuwa iwapo jimbo la Iringa mjini litapata mgombea mgombea mzuri hakuna upinzani katika jimbo hilo ila kama ugomvi wa madaraka utaendelea itakuwa ni kazi kupata mgombea wa CCM .
Alisema kuwa tabia ya baadhi ya wagombea kulazimisha kuendelea kugombea huku wakijua wamechuja ni moja kati ya sababu ya CCM kuendelea kuchokwa na wananchi na hivyo kuamua kuchagua wapinzani.
Kinana alisema kuwa tatizo la CCM kupoteza jimbo hilo ni uroho wa madaraka kwa wale ambao hawakubaliki kwa wananchi kosa ambalo kamwe CCM haitarudia kulifanya.
Kinana alihoji na kusema kuwa, kuna mitaa 150 katika jimbo la Iringa mjini ambapo ni mtaa mmoja pekee ndiyo CHADEMA waliuchukua, wakati huo huo kuna kata zaidi ya 17 ambapo CHADEMA walichukua kata moja kwenye uchaguzi. Sasa ni namna gani CCM ishindwe ubunge jimbo hilo hilo kama si tamaa za uongozi kwa baadhi ya wagombea.
Hivyo aliwataka viongozi hao wa CCM kujaribu kusoma alama za nyakati na iwapo watajua kuingia, basi wajifunze na kutoka kwani kuna wakati wa kuchokwa. Ni lazima wakubali kuondoka badala ya kung'ang'ania kugombea .
Pia katibu huyo aliwataka wana CCM kujifunza kujiuliza kwa wananchi wengine kama wanakubalika ama hawakubaliki badala ya kusimamia maamuzi yao ya kuingia kugombea bila kupendwa na wananchi na kuwa kosa lililofanyika mwaka 2010 kamwe halitajirudia tena.
" Ni mambo ya ovyo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya CCM ndio ambayo yamekigharimu chama na kuwa jimbo la Iringa mjini hakuna mpinzani ila wapo wanaotafuta kusikilizwa katika mambo yao na iwapo CCM itatenda mema kwa kusikiliza wananchi jimbo la Iringa mjini hakuna upinzani ila upuuzi ,rushwa ndani ya CCM na serikali yake ndio imekigharimu chama hicho "alisema
=================================================================================
Sehemu ya umati wa watu katika mkutano huo ulihutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana katika mji wa Nyololo, Mufindi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akionesha kadi 27 za wananchama wa Chadema waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini Nyololo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010. Kulia aliyevaa shati jeupe ni aliyekuwa Katibu wa Kata ya Igowole, Josephat Soda ambapo wengine ni miongoni mwa walio kuwa wafuasi wa Chadema.
Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kata ya Igowole, Josephat Soda akikabidhi bendera ya chama hicho kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya yeye na wenzie 26 kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akimkabidhi kadi ya CCM, Josephat Soda baada ya kutanga kujiunga na CCM katika mkutano huo.
Josephat Soda akielezea jinsi alivyoamua kuondoka Chadema na kujiunga na CCM, ambapo alisema amechoka na chama kilichosheheni uongo na ulaghai, ambapo alidai viongozi wa Chadema walitoa maagizo kuwa akope fedha za kujengea Mnara wa mwandishi wa habari Marehemu David Mwangosi, aliyeuawa wakati wa vurugu za CHADEMA na Polisi katika Mji wa Nyololo, ambapo walimuahidi kumtumia fedha zilizotumika kujenga mnara huo ahadi ambayo hadi sasa hawajaitimiza na anadaiwa na muuza simenti na muuza saruji alikokopa. Kutokana na maelezo yako, CCM imeamua kulipa madeni yote aliyokuwa akidaiwa ili kutunza heshima.
Wanachama wa CCM wakiwemo wale wapya kutoka Chadema, wakiapa kiapo cha utii cha CCM baada ya kukabidhiwa kadi wakati wa mkutano huo
Mfuasi wa CCM, Keneth Mwangosi, akiwa mbele ya gari lake alilolifanyia ukarabati wa kuvutia na mbele yake kuandika jina la Kinana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakichuma majani ya chai katika shamba la Unilver, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010, na pia kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi katika Jimbo la Mufindi Kusini, mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu (katikati) wakisaidia kuchuma majani ya chai katika shamba hilo la Unilve akiwa na viongozi wengine wa chama hicho
Kinana akisaidia kumwagilia maji miche ya miti alipokwenda kukagua bustani ya Vijana mjini, Kigamboni mjini Mafinga

Aliyewahi kuwa mgombea ubunge Jimbo la Kalenga wa Chadema kura za maoni, Sanga Abubakar akitangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo |