Aibu kwa jeshi la Polisi, kumbe mtandao wa wezi wa vifaa vya magari unajulikana

Pelekaroho

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
1,601
375
Aibu kwa Jeshi la Polisi, kumbe mtandao wa wezi wa vifaa vya magari unajulikana. Kuna madon hawa wao ndo wanajua wezi wote wa vifaa vya magari kutoka kila sehemu Dar es Salaam. Mtu utalazimika kununua vifaa vyako hata vikiwa na alama. Gerezani ndo terminal point kwa vifaa vyote. Kwa nini hili liendelee wakati jeshi la polisi likiendelea kulipwa kutokana na kodi zetu. Karibuni wadau tudadavue.

Chanzo ITV kipindi cha Uchunguzi Kamili. Leo saa nne usiku.
 
Hii mbona kitambo... Ukiibiwa sight mirror sa nne asubuhi mchana ukiibuka gerezani unauziwa kwa mara ya pili, bongo tambarare... Polisi daima wako likizo
 
Aibu kwa Jeshi la Polisi, kumbe mtandao wa wezi wa vifaa vya magari unajulikana. Kuna madon hawa wao ndo wanajua wezi wote wa vifaa vya magari kutoka kila sehemu Dar es Salaam. Mtu utalazimika kununua vifaa vyako hata vikiwa na alama. Gerezani ndo terminal point kwa vifaa vyote. Kwa nini hili liendelee wakati jeshi la polisi likiendelea kulipwa kutokana na kodi zetu. Karibuni wadau tudadavue.
Huu ni uchochezi dhidi ya jeshi la polisi, je ushahidi unao?
 
Nimekuta hiki kipindi kinafika mwisho mwisho ITV,sikupata bahati ya kusikia wakati wezi wanaojiwa, hivi kama gari limefungwa alarm hawa wanauwezo wa kudisable? Na kama wanaweza wanafanyaje? Alafu je kuna uwezekano kuiba taa bila kufungua milango ya magari na kuingia ndani?
 
Nafikiri hii taarifa italisaidia jeshi la polisi.....

Na pia polisi wasikae eneo moja kiasi cha kuzoeleka na kuanza kuoneana aibu
 
Inasemekana pia kwamba ukiibiwa kitu kwenye gari yako pale mlimani city (Laptop etc) na ukawahi faster Mabatini police, vitu vyako utavipata tena - ofcourse, kwa kuvinunua kwa mara nyingine.
 
Kwa taarifa yenu polisi are friends to criminal. Ukiona polisi kasanua dili ujue mgao umezingua.

Na ikiwa ni issue iliyokaa vibaya kiasi kwamba ukiisanua itakula na kwao tambua watakumaliza tu.

Mara ngapi tushaona polisi wakichukua posho zao kwa drug dealers, wauza gongo n.k?
Nliwahi pita kwenye junction moja mkoani Njombe, palipo na stand ya mabasi pale kwenye geti la kutokea penye traffic na vehicles wakt Mwingine,pembeni yake ndio soko kuu la unga na bangi na polisi wale wanajua kila kitu.
 
Aibu kwa Jeshi la Polisi, kumbe mtandao wa wezi wa vifaa vya magari unajulikana. Kuna madon hawa wao ndo wanajua wezi wote wa vifaa vya magari kutoka kila sehemu Dar es Salaam. Mtu utalazimika kununua vifaa vyako hata vikiwa na alama. Gerezani ndo terminal point kwa vifaa vyote. Kwa nini hili liendelee wakati jeshi la polisi likiendelea kulipwa kutokana na kodi zetu. Karibuni wadau tudadavue.
Sio mbaya kwa watukujipatia riziki kwa njia hiyo sababu umasikini umekithiri na wenye nazo hawawajali walalahoi,kwa hiyo ni kugawana kilichopo ili maisha yaendelee ,mkiwabana watu wakakosa mwanya wa kutafuta dona na dagaa iko siku wataingia msituni na kuunda kikosi kazi ,halafu hapatakalika kama Somalia na YEMENI .
 
Siku utakapokuwa mhanga wa janga hili utaelewa ni nini ninachojaribu kukisema.
 
Nimefuatilia kipindi cha ITV, wameongea na wezi wa vifaa vya magari, wakaongea na madalali ambao wao ni waunganishi kati ya madon(hawa ni wanunuzi wakubwa wa mali ya wizi na wana mtandao wa wezi wa vifaa hivi Dar es Salaam kote na wanaweza kukuletea vifaa vyako kama utatoa ushirikiano wanaohitaji ) na wahanga wa wizi huo.
 
Inasemekana pia kwamba ukiibiwa kitu kwenye gari yako pale mlimani city (Laptop etc) na ukawahi faster Mabatini police, vitu vyako utavipata tena - ofcourse, kwa kuvinunua kwa mara nyingine.
Mimi niliibiwa Mwenge laptop pamoja na ipad mbili, nikawahi polisi mabatini na mpaka leo sijapta chochote. Sanasana niliambulia kupata msamiati wanaotumia kwa suala kama hilo. Wanaita "PWEZA".
 
Back
Top Bottom