AIBU KUBWA: DC kukamatwa kwa rushwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AIBU KUBWA: DC kukamatwa kwa rushwa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lole Gwakisa, Jul 27, 2010.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  DC wa Kasulu ,Betty Machangu amekamatwa kwa Rushwa,Rushwa ya uchaguzi!!!
  UUUwi aibu gani hii?
  Kiongozi anayetakiwa kuwa mhimili wa mamlaka ya Rais Wilayani ndiye anakamatwa kwa rushwa.
  Huyu ni mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na uslalama katika wilaya yake ya Kasulu, leo ni mhalifu wa rushwa(ingawa bado kesi kwenda mahakamani)
  Aibu kubwa kwa serikali na kada yake ya uongozi.
  TZ DAIMA: DC Kasulu mbaroni kwa rushwa, alikuwa akitoa fedha, vitenge,asali,vipeperushi.TAKUKURU wapambana naye kwa saa 1
  NIPASHE: DC mgombea ubunge mikononi mwa TAKUKURU, pia wapambe,fedha zakamatwa(27/07/2010)
   
 2. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ukistaajabu ya Musa..... samaki anaanza kuoza kuanzia wapi?
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  kama hiyo utaiita rushwa basi TAKUKURU itakama karibu wagombea wote. Na TAKUKURU wataishia kushindwa, hatakutwa na hatia na wala hata jela hatakwenda, tena inawezekana hata ubunge atashinda. Subiri uone, pitia thread hii mwezi novemba
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,666
  Likes Received: 21,890
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu LG, ingekuwa aibu kama hii ni tabia mpya ndani ya CCM. Lakini haya ndiyo yaliyopo katika uendeshaji wa chaguzi za CCM na shughuli za serikali yake. Usishangae likatoka tamko kuwa "Hii ni ajali ya kisiasa tuu" Hiyo ndiyo CCM bwana. Haina tofauti na genge la uhalifu
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu nashindwa kusema kama hii ni aibu, kuna mambo mengine tunayafanya kila siku lakini hatuoni aibu kwa kuwa hayaandikwi magazetini. Can you call this thing shame or even scandal? Sasa kujua kama sio scandal wala shame utaona kama kuna mtu ataadhibiwa.
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mzee wa Bongo, ni aibu kubwa kimaadili kwa mtetezi wa haki na wanyonge kujikuta yeye yuko kundi hilohilo la rushwa.
  The stakes have been raised , hata Marigareta Sitta naye yuko mkumbo huu wa rushwa, sijui ni kwa ridhaa ya nani? mumewe?
  Hakika mnyonge hana chake.
   
 7. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nimekukubali bongolander maana nasikia yule afisa wa takukuru aliyekamata ndiye ameteremshwa cheo na kuhamishwa!!!!!!
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Siamini kama wagombea wengine wanafanya tofauti na wanaokamatwa. Kama ni kweli wanaokamatwa ndio pekee watoa rushwa ingekuwa heshima kubwa kwa chama kama wote ambao mashauri yao yamethibitishwa na Takukuru wangejiondoa kwenye kinyanganyiro cha kura za maoni
   
 9. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mbona wengine wanaruhusiwa kugawa vipeperushi wakati wengine hawaruhusiwi?
   

  Attached Files:

 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu ngoja tu tupate trend ya wa kukamatwa, maana sasa fununu ndo kwanza inaanza kujionyesha.
   
 11. M

  Mantaleka Senior Member

  #11
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wananchi waelewe kuwa, hii ndiyo miondoko iliyozoeleka kwa wote, sasa wanatafutana mumo kwa mumo, na wasio takiwa na kundi linalojiona lenyewe ndiyo lenyewe, watatangazwa na kudhalilishwa, lakini wenyewe wenyewe ng'o hautawasikia kukumatwa, dawa yao ni kuwanyima kura tu ! si tuna wajua !!
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Tazama kwa makini kama "watakaokamatwa" ni wale wapinga mafisadi.
  Then the whole thing will turn into an orchestrated move.
  Reflection ya hilo jambo linaanza kuonekana kwa kuhamishwa kazi kwa afisa TAKUKURU wa Moshi.Inaelekea huyo aliyekamatwa hakukusudiwa.
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  Pole dada yangu, nawe kumbe umo kwa rushwa?
  Aibu!!
   
Loading...