Ahukumiwa kiboko kimoja baada ya kumpa mwanafunzi mwenzake mimba

qaxemvule

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
231
120
Mahakama ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imetoa hukumu ya kuchwapwa kiboko kimoja mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Longoi wilaya hapo baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa shule hiyo.

Je, itakua fundisho kwa wengine au wataendelea wakijua adhabu ni rahisi?
 
Duuuu...mbona naona kama hakuna adhabu aliyopewa zaid ya kuambiwa jiandae kuwa baba mwanafunzi
 
Does not make sense...!! Mbona adhabu ni ndogo sana....?! Kweli kwa hukumu hiyo, wazazi wenye watoto wa kike watajichukulia sheria mkononi.
 
Inawezekana huyo aliemtia mimba mwenzie ni mtoto pia, meaning ana umri wa chini ya miaka 18..
 
Hiyo ndo point mkuu, kanuni ya adhabu 'penal code' , Education Act pamoja na Child Act zikisomwa kwa pamoja,zinakataza adhabu ya kifungo kwa mtoto mwenye umri wa miaka chini ya miaka 18,kwahiyo uenda huyo jamaa aliyemtia mimba mwanafunzi ni below 18 hivyo adhabu ya kiboko iko sahihi kabisa.
 
Lakni sio kiboko kimoja aise
 
Back
Top Bottom