Enzi hizo kwa ukame tunaopitia kwenye nchi hii,ingekuwa kila mtaa ni kelele za majenereta,tawala zilizopita,njia rahisi Ilikuwa ni kusema maji yamepungua kihansi kutokana na ukosefu wa mvua,na mgao kuanza.
Lakini hivi sasa ukame ni mbaya na Umeme upo kama kawaida.Nini kilikosekana kipindi hicho?
Lakini hivi sasa ukame ni mbaya na Umeme upo kama kawaida.Nini kilikosekana kipindi hicho?
Wadau, amani iwe kwenu.
Hivi mmejiuliza kwa nini mwaka huu hakuna zile story zilizozoeleka kipindi kama hiki kuwa Mabwawa yamepungua kina cha maji? Kwamba, mabwawa yanafunga uzalishaji wa umeme kutokana na kina chake kipungua na hivyo kuilazimu nchi kuwa na jitihada za kuwa na umeme wa dharura?
Aisee! Ule mkwara aliouchimba mwaka juzi Rais umesaidia sana kuondoa tatizo hilo. Tangu wakati ule sijasikia bwawa lolote likipungua kina cha maji licha ya kuwa nchi imekabiliwa na ukame kwa miezi kadhaa sasa. Katika mazingira yale ya kifisadi, watu wangetumia ukame huu kufanya biashara na serikali kama walivyotaka kutumia baa la njaa.
Mgawo wa umeme sasa ni historia nchini. Project nyingi za kuzalisha umeme zinafanya kazi na hivyo tuna umeme wa kutosha na wa uhakika. Nasikia bomba la gesi toka Mtwara linapitisha asilimia kumi tu ya uwezo wake. Hata hivyo, kiasi hicho kinachopitishwa kimemaliza kabisa tatizo la umeme nchini. Naamini kuwa bomba hilo likifanya kazi kwa asilimia 100 tutakuwa na umeme wa ziada na hivyo kuziuzia nchi jirani za Zambia, Msumbiji, Malawi, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC na nchi nyingine.
Kwa hakika Rais Magufuli ni shujaa na mkombozi. Kwa hii Political Will aliyonayo Rais wetu, Tanzania tutasonga mbele kwa haraka sana.