Umefurahiii?!!!! Akili yako haiko sawa wewe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameendelea kuweka rikodi iliyotukuka katika nyanja ya Elimu na katika kuendeleza kauli mbiu ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, amefunguwa Rasmi Chuo Kikuu Cha Kwanza Kijeshi Cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Hongera sana Kikwete, mpaka sasa tunaona juhudi zako na hii ni rekodi nyingine adhimu kwako na kwa Taifa.
Kwa hakika Elimu pekee ndio itayompa Maisha Bora kila Mtanzania. Na unafanya kweli!
Kimejengwa kwa Sh.ngapi na chanzo cha fedha hizo ni nini?
Kitaendeshwa kwa budget ipi?
Kitasomesha watu gani na wangapi kwa mara moja?
Anasubiri aage dunia ndio aamue, muda wake unaisha, tunamkumbusha, zile meli nyasa, victoria na tanganyika, na kigoma bado haijawa dubai na.....du ukianza kutaja zile ahadi unapata degedege kwa jinsi zilivyo changa la macho. Hongera presidaa kwa kutupiga kipapaibig up presidaa, umejitahidi.
Binafsi naamini jk anaweza kufanya mengi zaidi, hajaamua tu kufanya.
Naamini hakuna linalo mshinda ila ni uamuzi wake tu unahitajika.
Zomba hana uwezo au uelewa wa kuweza kujibu haya maswali. Yeye anaposikia chuo kikuu cha kijeshi, mawazo yanamtuma kwamba ni Military University. Kumbe hajui kwamba tuna hata chuo kikuu cha polisi kurasini na chuo kikuu cha magereza ukonga. Hapa haina maana kwamba ni universities, bali katika mafunzo yao ya kijeshi vyuo hivyo ndiyo vinatoa mafunzo advanced. Haina maana ukitoka hapo unakuwa na digrii au diploma ya kijeshi, ya polisi au ya magereza.zomba, unaweza kutupa details zaidi kuhusu hicho chuo kikuu kipya cha kijeshi? i.e kiko affiliated, na chuo gani? funding zinatoka ndani au kwa nje, na kama ni nje ni nchi gani? kinajengwa/kimejengwa wapi? na kitachukuwa wananfunzi wangapi? shukrani.