Nilipoanzisha thread hii sikua na maana ya kuhukumu mawazo na hisia za Ahmed Rajab lakini ukweli lazima ujisimamie wenyewe,anapodai kwenye
moja ya makala zake kuwa uamusho hawahusiki na vurugu na vitendo vya uchomaji makanisa alikuwa anamsemea,hamjui kuwa kushabikia mambo kama haya ya uvunjifu wa amani mbele yeti kuna dhahama kubwa ,basi siku moja tutarajia yale ya al-shabab,boko haram hata tuareg guerilla kule mali.
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini sana makala za mwandishi wa habari
Ahmed Rajab katika gazeti la Raia mwema zinazozungumzia masuala ya
kisiasa zaidi nilichogundua kuwa huyu mwandishi ni mtu anayeshabikia
sana kuvunja muungano na kubariki mienendo jumuia ya uamusho,z'bar
je huyu jamaa ni mzalendo au mchochezi,naomba tumjadili.
We ni mjinga tu! Na huelewi ila ipo siku utaelewa. Siku zote unapenda kuona habari unazozitaka wewe tena zile za kupikwa na nadharia zaidi,hapo roho na akili yako hutua kwa utulivu.Habari za halihalisi huzitaki kwakuwa kwako ni uchochezi na machukizo makubwa! Rajab anasema kweli. Kamakweli wewe unapenda haki na kweli hebu nipe chanzo cha kuibuka Al-shabaab wanaoitwa magaidi.