Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Ahmadinejad: Hakuna dola lolote linaloweza kulipigisha magoti taifa la Iran
?Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hakuna dola wala kundi lolote linaloweza kulilazimisha taifa la Iran lifanye kitu kinyume na matakwa yake.
Mheshimiwa Rais amesema hayo leo mbele ya umati mkubwa wa wananchi wa mji wa Sarayan wa kaskazini magharibi mwa mkoa wa Khurasani Kusini hapa nchini na kuongeza kuwa, maadui na hasa madola ya kibeberu hayawezi kulifanya taifa la Iran lipige magoti mbele ya njama na hila zao za kiadui kwani taifa hili linaloongozwa na mwanachuoni mcha Mungu halina sifa tena ya kuwa mtumwa wa mataghuti na mashetani na limeamua kikwelikweli kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu tu.
Amesema, leo hii mabepari wasio na ustaarabu ndio wanaodhibiti taasisi na vituo vikuu na muhimu duniani hususan serikali ya Marekani na waitifaki wake na lengo lao ni kuyafunga minyororo mataifa yote ya dunia ili yaweze kuyadhibiti chini ya ubeberu wao. Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa, tatizo kubwa la jamii ya mwanadamu katika kipindi chote cha historia hadi leo hii ni kwamba kuna baadhi ya watu wachache ambao badala ya kuwavutia watu upande wa kuwa watumwa wa Mwenyezi Mungu tu, wanawavuta kuwa watumwa wao binafsi.