Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 427
- 666
Wakija mbele ya Wananchi wanaonekana kama malaika lakini wanapoondoka huonekana kama ibilisi. Hiki ndicho unachoweza kusema maisha baada ya kampeni na kumalizika kwa uchaguzi.
Ni jambo la kawaida kwa Wanasiasa wanaogombea kunadi sera zao kwa wananchi ingawa wengi wao huishia mitini baada tu ya kutangazwa kushinda uchaguzi.
Si jambo la kushangaza ukapita maeneo mengi kukutana na changamoto ya barabara, shida ya maji, na hata uchakavu wa miundombinu.
Lakini leo jicho hili limeamua kupiga kambi kwa baadhi ya maeneo kuona uhalisia ulivyo wa maendeleo.
Daudi Kashengena (si jina lake halisi), Mkazi wa Makoka anasema barabara hiyo imekuwa kero kubwa hasa katoka kipindi cha mvua, lakini ahadi za mgombea Ubunge wa jimbo hilo amekuwa akinadi kutatua changamoto hiyo bila mafanikio.
‘‘Mimi ni bodaboda, lakini inapofika suala la Makoka mbele ya shule siwezi kwenda kwa buku kwa sababu ya barabara yake sio nzuri, na mara nyingi usiku ni mara chache huwa siendi’’
Wakati kukiwa na kilio cha barabara huko, wakazi wa Tabata Jimbo la Segerea kilio cha huduma ya maji ni kama hakijasikika, na kikisikika basi ni kwa muda tu.
BARABARA NA JINSI MAGARI YANAVYOPITA JIMBO LA UKONGA
Pia soma - Barabara ya Mbezi Makabe kwa Pesapesa kuwa mbovu kiasi hiki Mbunge, Diwani, Mkuu wa Mkoa na Wilaya wapo kweli?
PICHA: MWANANCHI DIGITALNi moja ya barabara eneo la Tabata Bima barabara inayounga kuelekea Kimanga, na nyingine ikielekea Gongo la Mboto.
“Kwetu tumeshazoea wakija wanaahidi wanaondoka” hii ndio kauli ya wengi katika Jimbo la Ubungo wakazi wanaotumia Barabara ya Makoka ambayo imekuwa kikwazo kwa wananchi hali inayofanya kupata shida ya usafiri na wakati wa mvua hali inazidi kuwa mbaya zaidi.
Bi. Tesha aliyezungumza kwa sharti la kutotaja majina yake kamili anasema ameishi eneo hilo kwa zaidi ya miaka 40 lakini suala la maji limekuwa si la kuacha kuzungumziwa na wagombea kila uchaguzi.
Anasema kuna wakati wanakaa hadi wiki tatu bila maji, badala yake wanaweza kupata huduma hiyo kwa siku moja na tena usiku, asubuhi hayapo tena.
Swali linalobaki ni je Kwanini ahadi nyingi zimekuwa hazitekelezeki?
Moja ya mchambuzi wa siasa hapa nchini ambaye alipenda kutambulishwa kwa jina moja la Faraja anasema wakati mwingine wagombea wengi hunadi sera na ahadi zao kwenye mikutano ambapo si katika vipaumbele vya ilani ya chama husika baada ya kushinda uchaguzi.
Anasema miongoni mwa sababu zingine ni uchache wa rasilimali na bajeti ambapo ameeleza chama kinaweza kuahidi miradi katika ilani, lakini rasilimali hazitoshi, hivyo ahadi zote za chama hazitimizwi.
Katika kudodosa zaidi anaeleza wakati mwingine, ni ubinafsi wa viongozi kutotekeleza na wakati mwingine kutumia fedha ndogo tofauti na ile inayotengwa na serikali na matokeo yake hukarabatiwa barabara chache na kwa kiwango kisichoridhisha.
Huku Jimbo la Ukonga, kilio ni cha barabara za ndani, Wananchi wakitaka kurekebishwa na ikiwezekana kuwekwa lami ili kurahisisha shughuli zao za kiuchumi.
Mkazi mmoja anasema Mbunge aliyekuwepo awali aliahidi kumaliza changamoto hiyo ingawa hakufanikiwa, akisema mategemeo ni kwa mbunge mpya je atafanikisha kutatua changamoto hiyo?
Pamoja na kwamba uchaguzi umekamilika vipo vinavyosubiriwa ikiwa je vitatekelezeka ikiwemo ahadi zilizokuwa kwenye ilani ya chama tawala kilicho madarakani kwa sasa.
INAONESHA ILANI YA CCM (CREDIT: CCM WEBSITE)Ikiwa ahadi zitakuwa zenye kutekelezwa ni Dhahiri, Tanzania iliyoendelea kwa wananchi itafikiwa, na changamoto kutatuliwa, na si kuwa na viongozi wenye kunena bila kutenda.
Ni jambo la kawaida kwa Wanasiasa wanaogombea kunadi sera zao kwa wananchi ingawa wengi wao huishia mitini baada tu ya kutangazwa kushinda uchaguzi.
Si jambo la kushangaza ukapita maeneo mengi kukutana na changamoto ya barabara, shida ya maji, na hata uchakavu wa miundombinu.
Lakini leo jicho hili limeamua kupiga kambi kwa baadhi ya maeneo kuona uhalisia ulivyo wa maendeleo.
Daudi Kashengena (si jina lake halisi), Mkazi wa Makoka anasema barabara hiyo imekuwa kero kubwa hasa katoka kipindi cha mvua, lakini ahadi za mgombea Ubunge wa jimbo hilo amekuwa akinadi kutatua changamoto hiyo bila mafanikio.
‘‘Mimi ni bodaboda, lakini inapofika suala la Makoka mbele ya shule siwezi kwenda kwa buku kwa sababu ya barabara yake sio nzuri, na mara nyingi usiku ni mara chache huwa siendi’’
Wakati kukiwa na kilio cha barabara huko, wakazi wa Tabata Jimbo la Segerea kilio cha huduma ya maji ni kama hakijasikika, na kikisikika basi ni kwa muda tu.
BARABARA NA JINSI MAGARI YANAVYOPITA JIMBO LA UKONGA
Pia soma - Barabara ya Mbezi Makabe kwa Pesapesa kuwa mbovu kiasi hiki Mbunge, Diwani, Mkuu wa Mkoa na Wilaya wapo kweli?
PICHA: MWANANCHI DIGITAL
“Kwetu tumeshazoea wakija wanaahidi wanaondoka” hii ndio kauli ya wengi katika Jimbo la Ubungo wakazi wanaotumia Barabara ya Makoka ambayo imekuwa kikwazo kwa wananchi hali inayofanya kupata shida ya usafiri na wakati wa mvua hali inazidi kuwa mbaya zaidi.
Bi. Tesha aliyezungumza kwa sharti la kutotaja majina yake kamili anasema ameishi eneo hilo kwa zaidi ya miaka 40 lakini suala la maji limekuwa si la kuacha kuzungumziwa na wagombea kila uchaguzi.
Anasema kuna wakati wanakaa hadi wiki tatu bila maji, badala yake wanaweza kupata huduma hiyo kwa siku moja na tena usiku, asubuhi hayapo tena.
Swali linalobaki ni je Kwanini ahadi nyingi zimekuwa hazitekelezeki?
Moja ya mchambuzi wa siasa hapa nchini ambaye alipenda kutambulishwa kwa jina moja la Faraja anasema wakati mwingine wagombea wengi hunadi sera na ahadi zao kwenye mikutano ambapo si katika vipaumbele vya ilani ya chama husika baada ya kushinda uchaguzi.
Anasema miongoni mwa sababu zingine ni uchache wa rasilimali na bajeti ambapo ameeleza chama kinaweza kuahidi miradi katika ilani, lakini rasilimali hazitoshi, hivyo ahadi zote za chama hazitimizwi.
Katika kudodosa zaidi anaeleza wakati mwingine, ni ubinafsi wa viongozi kutotekeleza na wakati mwingine kutumia fedha ndogo tofauti na ile inayotengwa na serikali na matokeo yake hukarabatiwa barabara chache na kwa kiwango kisichoridhisha.
Huku Jimbo la Ukonga, kilio ni cha barabara za ndani, Wananchi wakitaka kurekebishwa na ikiwezekana kuwekwa lami ili kurahisisha shughuli zao za kiuchumi.
Mkazi mmoja anasema Mbunge aliyekuwepo awali aliahidi kumaliza changamoto hiyo ingawa hakufanikiwa, akisema mategemeo ni kwa mbunge mpya je atafanikisha kutatua changamoto hiyo?
Pamoja na kwamba uchaguzi umekamilika vipo vinavyosubiriwa ikiwa je vitatekelezeka ikiwemo ahadi zilizokuwa kwenye ilani ya chama tawala kilicho madarakani kwa sasa.
INAONESHA ILANI YA CCM (CREDIT: CCM WEBSITE)