Tangopori
JF-Expert Member
- May 11, 2012
- 1,629
- 1,282
Inabidi atueleze hizi fedha atazipata wapi ndani ya miaka mitano na bado barabara zijengwe, watumishi walipwe mishahara, kila kijiji kipate 50M e.t.c
Au ndo atakimbilia kwa wafadhili akiondoka deni la taifa liwe limefikia 200Trillion?
Sawa na baba wa familia ajivunie kuijengea familia nyumba ya 100M huku amewaacha na deni la 100M
================================
CHANZO: NIPASHE
Au ndo atakimbilia kwa wafadhili akiondoka deni la taifa liwe limefikia 200Trillion?
Sawa na baba wa familia ajivunie kuijengea familia nyumba ya 100M huku amewaacha na deni la 100M
================================
Zahanati kila kijiji: Sh. trilioni 24.96, Kituo cha afya kila kata:, Sh. trilioni 19.7 Jumla makadirio: Sh. trilioni 44, Ni 44% ya bajeti ya serikali ya miaka mitano. Ahadi: Zahanati kila kijiji, kituo cha afya kila kata, hospitali kila wilaya pamoja na hospitali ya Rufaa kwa kila mkoa.
Ni wakati wa kampeni na ni wakati wa kila mgombea kutoa ahadi kwa wapigakura kuhusu mambo atakayoyapa kipaumbele katika miaka mitano endapo atapata ridhaa ya wananchi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, katika mikutano yake ya kampeni, ameahidi kujenga zahanati katika kila kijiji nchini, kituo cha afya katika kila kata, hospitali kila wilaya na hospitali ya rufaa kila mkoa, endapo atapata ridhaa ya kuwa rais wa awamu ya tano, ili kuboresha huduma za afya nchini.
Gazeti hili limetafuta gharama ya kutekeleza ahadi hii kubwa kabisa kuwahi kutolewa na mgombea urais tangu kuanza mfumo wa vyama vingi nchini.
Katika kutafuta na kuchambua uhalisia wa ahadi hii, gazeti hili limepata taarifa za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zinazoonyesha kwamba gharama za kujenga zahanati moja ya kijiji ni takribani Sh. bilioni 1.3 hadi kukamilika kwake.
Aidha, ujenzi wa kituo cha afya ambacho majengo yake yana sifa zinazostahili, unakadiriwa kugharimu Sh. bilioni 5.5 hadi kukamilika kwake.
Kwa upande wa ujenzi wa hospitali yenye hadhi ya wilaya, ujenzi wake unakadiriwa kugharimu kiasi cha Sh. bilioni 30 ili majengo yake yakamilike na kutumiwa kwa shughuli za kutoa huduma za afya.
Makisio ya Wizara ya Afya ambayo Nipashe iliyapata, ujenzi wa hospitali ya mkoa wowote hapa nchini, unakadiriwa kutumia Sh. bilioni 50 na hospiatli moja ya rufaa inagharimu Sh. bilioni 80.
Kwa mujibu wa Kitengo cha Uhandisi katika wizara hiyo, gharama hizo ni makisio na zinaweza kupungua au kuongezeka kwa asilimia tano kutegemea eneo na ushindani wa manunuzi husika.
Makadirio ya gharama
Gazeti hili limejikita tu katika ahadi kuu mbili, ujenzi wa zahanati kila kijiji na ujenzi wa kituo cha afya kila kata, nchi nzima, kama alivyoahidi Dk. Magufuli katika kampeni zake.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Tanzania ina vijiji 19,200. Kwa sababu hiyo, Ili kuvijengea zahanati kwa kila kimoja, zitahitajika Sh. trilioni 24.960, sawa na Dola za Marekani bilioni 12.48, endapo mradi huu utatekekezwa katika kipindi cha miaka mitano.
Kwa kuwa haya ni makadirio tu, gharama hizi zinaweza kupungua au kupaa zaidi katika kipindi hicho kulingana na mfumuko wa bei au thamani ya Sarafu ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.
Gazeti hili limekadiria thamani ya Shilingi kwa Dola ya Marekani kuwa ni Sh. 2,000, japo mpaka sasa thamani halisi katika soko ni zaidi ya kiwango hicho. Hii ina maana kwamba zahanati moja itagharimu Dola za Marekani 650,000(Sh. bilioni 1.3) na hivyo basi kwa vijiji 19,200, jumla itakuwa Dola za Marekani bilioni 12.48(Sh. trilioni 24.960).
Hii ni sawa na wastani wa Sh. trilioni 4.992 sawa na dola za Marekani bilioni 2.496 kwa mwaka endapo mradi huu utatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ya awamu ya tano ya Dk. Magufuli. Idadi hii inaweza kupungua kidogo kutokana na ukweli kwamba baadhi ya vijiji tayari vina zahanati, japo kwa uchache ukizingatia hali ya huduma za afya nchini.
Kiasi hiki cha fedha kwa mwaka ni sawa na asilimia 22 ya bajeti yote ya serikali iliyowasilishwa bungeni katika mwaka wa fedha wa 2015/16.
Katika mwaka wa fedha wa 2015/16 Serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh. trilioni 22.495.
Fedha zitakazohitajika kwa mwaka kujenga zahanati tu kwa kila kijiji ni mara sita ya bajeti ya Wizara ya Afya ya mwaka 2015/16.
Katika mwaka wa fedha wa 2015/16, Serikali ilitenga kiasi cha Sh. bilioni 813.976 (sawa na Dola za Marekani milioni 400) kwa ajili ya bajeti yote ya Wizara ya Afya.
Kituo cha afya kila kata
Kwa mujibu wa Tamisemi, idadi ya kata zote nchini ni 3,802. Kwa sababu hiyo, ili kujenga kituo cha kisasa cha afya kwa kila kata, Dk. Magufuli atahitaji kiasi cha Sh. trilioni 19 (Dola za Marekani bilioni 9.505) katika miaka mitano endapo serikali yake itatekeleza mpango huu kabambe.
Kwa mujibu wa makadirio kutoka Wizara ya Afya, kujenga kituo cha afya cha kisasa kinachoweza kuhudumia kata, gharama yake ni wastani wa Sh. bilioni tano (Dola za Marekani milioni 2.5.)
Hii gharama ni sawa na wastani wa Sh. trilioni 3.802 kwa mwaka katika miaka mitano ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huu.
Jumla ya fedha inayotakiwa katika kujenga zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata inakadiriwa kuwa Sh. trilioni 43.960 (Dola za Marekani bilioni 21.985) kwa miaka mitano (sawa na asilimia 40 ya bajeti ya serikali ya miaka mitano) kwa kutumia kipimo cha bajeti ya mwaka 2015/16.
Ikumbukwe kwamba bajeti ya serikali hupanda kila mwaka kulingana na mahitaji halisi ya kiuchumi na matumizi ya serikali.
Gazeti hili limejikita tu katika ahadi kuu mbili, ujenzi wa zahanati kila kijiji na ujenzi wa kituo cha afya kila kata, nchi nzima, kama alivyoahidi Dk. Magufuli katika kampeni zake.
CHANZO: NIPASHE