mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Gazeti la Nipashe, Alhamisi Aprili 28, 2016 limeripoti kuwa Jaji Salome Kaganda (Kamishina wa maadili Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma) amewapa Makatibu Tawala wa Mikoa ( RAS) wapya siri ya kutumbuliwa na Rais John Pombe Magufuli katika utumishi wa umma.
Siri yenyewe ni kufuata, bila kigugumizi, kifungu namba tatu cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, waliyoitia sahihi wakati wanakula kiapo.
Kifungu kinasomeka "Sitatumia cheo changu au wadhifa wangu kwa maslahi binafsi, ya familia yangu, ndugu zangu au marafiki zangu isipokuwa kwa maslahi ya umma".
Nalileta kwenu wanaJF na tafsiri yangu pana kwamba kifungu hicho kinamgusa kila mmoja wetu. Kila tunaloliwaza na kulitenda tujiulize ni kwa manufaa ya nani. Hii hasa ukiwa na majukumu ya kutekeleza yanayowagusa wengine. Kwa mfano unapo'post' mada humu lengo liwe kwa jamii siyo ubinafsi.
TUACHANE NA UMIMI