mkafrend
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,047
- 1,503
JOHN MAGUFULI AWAAHIDI AJIRA WALIOANGUKA KURA ZA MAONI CCM.
Mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, akihutubia mkutano wa kampeni mjini Tunduma mkoa wa Songwe jana. Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amewapooza wagombea wa chama hicho waliodondoshwa kwenye kura za maoni kwa kuwaahidi atawapa ajira hivyo kuwataka wasikikimbie chama hicho.
Hali kadhalika, Dk. Magufuli amewataka wana - CCM hao kutoendeleza makundi kwa kuwa yatahatarisha ushindi wa chama hicho. Aidha, amewaombea msamaha wagombea wa Majimbo ya Sumbawanga Mjini, Kwela, Kalambo mkoani Rukwa na Momba mkoani Sogwe."Nawaomba muwasamehe saba mara sabini kwa kuwa hawachagui malaika bali binadamu ambaye siyo mkamilifu," alisema Dk. Magufuli. Alisema yawezekana yapo ambayo hawakuyatekeleza kama inavyotakiwa na makosa mengine ambayo yamekuwa kinyume na matarajio ya wananchi, lakini anawahitaji afanye nao kazi na ahadi zote watakazoahidi watazitekeleza kwa maendeleo endelevu ya wananchi.
ATAKA MAKUNDI YAVUNJWE
Akiwa Jimbo la Kwela ambalo mgombea wake ni Ignus Malocha, alisema kura za maoni zimeisha na kinachotakiwa ni kuvunja makundi na kufanya kazi ya kuipa ushindi CCM. "Inawezekana mbunge wenu hakufanya hadi mlipotarajia, namuombea msamaha kweli kweli, nipeni, huyu ni binadamu hatuchagui malaika, mchagueni Malocha msihadaishwe na maneno mengi," alisisitiza. Akiwa Jimbo Kalambo ambalo mgombea wake ni Josephat Kandege, alisema waliobwagwa kura za maoni hawapaswi kulalamika na kuacha kuunga mkono mgombea aliyepita, kwani akiwa rais nafasi za kazi zitakuwa nyingi kila mmoja atapata.
"Nakwenda kuwa rais, nafasi za kazi ni nyingi sana. Mligombea kwa kuwa mnataka kufanya kazi, nitawapa kazi, lakini hakikisheni huyu anashinda," alisema.
Katika Jimbo la Momba ambalo mgombea wake ni Dk. Lucas Siyame, alirejea ombi la msamaha kwa wananchi hao kwa kuwa mgombea huyo alihimiza ujenzi wa barabara ya Sumbawanga hadi Tunduma, lakini kwa sababu ambazo hazieleweki walimuangusha.
"Tunaambiwa tusamehe saba mara sabini, kama kuna dhambi aliifanya msameheni na ikifika Oktoba 25, mpe kura za ndiyo," alisema. Alisema wagombea wengine wasiwe na shaka kwani serikali ya awamu ya tano itakuwa na nafasi nyingi za wachapakazi na waadilifu na kutokana na nia yao ya kutumikia watu, hawatakosa nafasi hizo.
"Licha ya jitihada za wakati huo, lakini mkampiga chini, ila namuombea msahama, mrudisheni wakati huu nifanye naye kazi, tunahitaji maendeleo bora kwa wote na hayo yataletwa na mafiga matatu kwa maana ya diwani, mbunge na rais," alisema.
Akiwa Jimbo la Sumbawanga Mjini ambalo mgombea wake ni Aeshi Hilary, pia aliwaomba wananchi wafute makosa na kuanza upya kwa kumpa kura za ushindi. Akiwa Jimbo la Mpanda Mjini, alitoa ahadi ya kazi kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kipindi kilichopita kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Said Arfi, na kuangushwa kwenye kura za maoni za CCM, huku akisema alikokuwa alikuwa amekosea njia.
"Kazi zipo nyingi nitakuwa rais wa nchi hii, kazi zipo nyingi wala usiwe na shaka, sitakosa nafasi ya kukupa, najua uwezo wako katika kazi," alisistiza.
Mimi nakumbusha tu, hongera sana JPM kwa usimamizi thabiti wa Serikali unayoingoza