BIN BOR
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 1,013
- 407
1. Mabasi ya mwendokasi (BRT), yalizinduliwa siku chache kabla ya uchaguzi 2015. WAPI? Wanadai kuhangaika na nauli wakati ukweli ni kuwa vituo havijakamilika kujengwa, mfano Morocco na Ubungo bado ni mapagala. Mikoa mingine mnaonaje, maana huko nako kunahitaji usafiri bora.
2. Tutawajali bodaboda na mama lishe. Madereva wa bodaboda (Dar) sasa wanazisoma namba za bodaboda zao kuliko wakati mwingine wowote. Vituo vikuu vya kukamata ni mataa ya Veta, Ubungo na Fire (Nimeweka kimoja kwa kila wilaya. Mikoa mingine mtupe hali bodaboda wa huko.
3. Kuwasaidia wasanii - hii wameifanyia kazi kwa kutangaza mrahaba kwa wasanii kutoka radio. Niambie nani kalipwa na kapewa ngapi?
4. Umeme hautakatika ovyo ovyo - nani kasema? Bado tunafanya kazi kwa kuvizia saa ngapi watakata na watakuja na visingizio gani. Kutoka mikoa mingine mtujulishe pia kuhusu umeme.
5. Mahakama ya mafisadi - Takukuru imewapa Lake Oil miezi mingapi sijui, walipe. EPA style. Wa mikoa mingine msiongelee hili, tuambieni bei ya mafuta huko ni kiasi gani?
6. Cement itauzwa elfu sita yaani 6,000/=. Wamakonde wenyewe hawamuelewi Ngosha hadi sasa. Yaani kiwanda ajenge Aliko bei apange John! Na bei hii ilitangazwa bila kujali ni Ntalwa au Bukoba. Na tarehe ya bei mpya ilisemwa Januari 2016. Kwa sauti kubwa - "kuanzia mwezi wa kwanza......2016......"
7.Milioni 50 kila kijiji - sijui ni za nini lakini wakileta sawa tu. Lakini wamebadili gia hewani wanasema ni mkopo. Japo hawakusema hivyo awali, lakini nakumbuka bilioni za JK, ziliishia wapi. Huko Kigoma mlipata? Wamesema wiki ijayo watawaletea.
8. Kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kukataza safari za nje bado hakujasaidia kushusha bei ya mkate dukani. Na usije hapa na pumba zako kuwa ati jamaa ana siku chache tu ikulu. Hizi siku chache chache ndio ukiunganisha unapata miezi na miaka.....
Sijachoka kuongezea hapa ahadi hewa, nakuachia nafasi na wewe uongezee nyingine ulizosikia......