Agundua mumewe ana mtoto wa nje baada ya ndoa

Aurora

JF-Expert Member
May 25, 2014
7,308
5,270
Habari zenu wapendwa,

Rafiki yangu yuko matatizoni, aliolewa mwaka juzi na kubahatika kupata mtoto mmoja, kipindi chote cha uchumba wao mwanaume alimwambie (rafiki yangu) kuwa hana mtoto wa nje, sasa wiki iliyopita mume wake ndio akamkalisha chini na kumwambia kuwa ana mtoto ambae yuko kidato cha tatu.

Rafiki yangu alilia sana, na toka siku hiyo hadi sasa hivi, ametokea kumchukia mume wake coz anasema hakuwa akitaka kuolewa na mwanaume mwenye mtoto tayari, ana chuki kwa huyo mtoto maana hataki hata kukutanishwa nae, alijaribu kumwambia mama yake lakini anasema she is not on her side.

Naombeni ushauri wenu ili niweze kumshauri maana amekuwa mtu wa kulia tu,hadi pressure imekuwa inampanda, kazi anaharibu, ikifika muda wa kutoka kazini, hatamani hata kurudi nyumbani, yani hayuko sawa kabisa.

Asanteni
 
Sasa analia lia nini huyo mpuuzi kwani aliyezaliwa ni binadamu sio kitu cha ajabu.mwambie ili aondokane na pressure na stress aondoke tu.
 
Kosa la jamaa ni kutokumwambia mapema tu kuwa ana mtoto wa nje sasa kwa nini yeye huyo mwanamke amchukie hadi mtoto ama ndiyo asili ya ule usemi kuwa mama wa kambo si mama..... Yeye apambane na jamaa ake na keshazalishwa mtoto mmoja tayar na hatowezi geuza ukweli uwe uongo yaani ndo tayar jamaa ana mtoto ye awe mpole tu....
 
Huyu itakua dish limeyumba kwani kua na mtoto ni dhambi.....mbna wa2 wanaoa wanawake wenye watoto n maisha yanasonga tu muhimu ni upendo.....kma hamtaki huyo mtoto anangangania ndoa ya nini c asepe mana huwezi kupenda bwana usipenda mtoto wke ni unafiki tu
 
Habari zenu wapendwa,
Rafiki yangu yuko matatizoni, aliolewa mwaka juzi na kubahatika kupata mtoto mmoja, kipindi chote cha uchumba wao mwanaume alimwambie (rafiki yangu) kuwa hana mtoto wa nje, sasa wiki iliyopita mume wake ndio akamkalisha chini na kumwambia kuwa ana mtoto ambae yuko kidato cha tatu.

Rafiki yangu alilia sana, na toka siku hiyo hadi sasa hivi, ametokea kumchukia mume wake coz anasema hakuwa akitaka kuolewa na mwanaume mwenye mtoto tayari, ana chuki kwa huyo mtoto maana hataki hata kukutanishwa nae, alijaribu kumwambia mama yake lakini anasema she is not on her side.

Naombeni ushauri wenu ili niweze kumshauri maana amekuwa mtu wa kulia tu,hadi pressure imekuwa inampanda, kazi anaharibu, ikifika muda wa kutoka kazini, hatamani hata kurudi nyumbani, yani hayuko sawa kabisa.

Asanteni
ucmsingizie rafiki hii story ni yak mwenyewe.. sema unatafuta pa kutokea.. umekwama jikwamue
 
Mwambie kuna wengine wanazaa nje ya ndoa wakiwa tayari wapo kwenye ndoa,
Aache mambo yake bhana
Inaonekana huyo mwanamke anapenda kujiweka juu ya mmewe au kujiona wa thamani kuliko mmewe
Ana kipato kikubwa zaidi ya mmewe?
 
Sawa jamaa alikosea kumficha. Lakini swali langu ni kwamba huyo mtoto anahusiana nini na ndoa yake?? Ye aendelee na maisha yake tu na huyo mtoto ampende kama anavyopenda baba ake na ndoa yako itakuwa yenye furaha na amani
 
Habari zenu wapendwa,
Rafiki yangu yuko matatizoni, aliolewa mwaka juzi na kubahatika kupata mtoto mmoja, kipindi chote cha uchumba wao mwanaume alimwambie (rafiki yangu) kuwa hana mtoto wa nje, sasa wiki iliyopita mume wake ndio akamkalisha chini na kumwambia kuwa ana mtoto ambae yuko kidato cha tatu.

Rafiki yangu alilia sana, na toka siku hiyo hadi sasa hivi, ametokea kumchukia mume wake coz anasema hakuwa akitaka kuolewa na mwanaume mwenye mtoto tayari, ana chuki kwa huyo mtoto maana hataki hata kukutanishwa nae, alijaribu kumwambia mama yake lakini anasema she is not on her side.

Naombeni ushauri wenu ili niweze kumshauri maana amekuwa mtu wa kulia tu,hadi pressure imekuwa inampanda, kazi anaharibu, ikifika muda wa kutoka kazini, hatamani hata kurudi nyumbani, yani hayuko sawa kabisa.

Asanteni
Mwambie huyo rafikiyo aache utoto, aendelee na kuzaa watotot wake na maisha yanaendelea.
Akioenda kulipiza kisasi akazae nje na yeye.
 
Mpenzi Mtoa Mada,
Huyo rafiki yako (wewe binafsi I guess) hayajui maisha. Tuombe Mungu amjalie utulivu ili ajifunze. Wanaume wenye nia safi siku zote hufunguka wenyewe kwa vipenzi vyao. Iwe ni kabla au baada ya kufunga ndoa. Huyo mume ni muungwana na I can tell anampenda mkewe kuliko tunavyodhani na ndo maana kamkalisha chini na kumjulisha ili wajipange pamoja as a family.
Tatizo kubwa la baadhi ya madada wa kisasa ni kwamba ukiona unapendwa sana na mumeo basi unajiona unapendwa na wanaume wote duniani. That's wrong.
Kama haamini maneno haya mwambie aendelee kuikuza issue aone mwisho wake kama si majuto na shinikizo kubwa la damu.
Ni mtoto huyo si mke.
Mwambie awaulize waliokataa pema kwa sababu za kukurupuka wamwamwambie urahisi wa kupata mume anayejali huko mtaani.
 
Back
Top Bottom