Agizo la Rais kunyang'anywa Passport Mkandarasi wa Maji

Sijasikiliza yote ila nimeona sehemu anasema hakuna sehemu Mkandarasi anapewa pesa ndiyo afanye kazi. Ina maana ile dhana ya advance payment kwa wakandaras haipo duniani au kajitoa akili?

Anyway, mm sijamsikia from the beginning lkn naamini kabisa Kuna uwezekano wa uzembe kote kote. Mkuu ktk mirad hii serikali nayo ina sarakasi zake za ajabu sana.
Sikiliza kwanza yote uelewe ndo uchangie
 
Acha uongo ww
Ukiharibu nchi za watu watakukamata wewe na sio passport yako
wakshakukamata utatorokaje?
Umeelewa nilichoandika? Wanachukua kwanza passport yako huku unahojiwa au upo mahabusu au upo nje kwa dhamana lakini lazima wachukue kwanza pass yako. Mwulize Eddo Kumwembe akusimulie.
 
Rais Magufuli kama huo ndo udikiteta naomba uzidishe mara 100 nshaupebda sasa jamn endelea tu napenda mambo kama hayo
 
Wanaoteseka na ukosefu wa maji ni wananchi hawa hawa
Leo maji yasipokuwepo kilio kwa selikal sasa mnateta wanasababsha ukisefu ili iweje
 
Inashangaza mbongo mwenzangu amekomaa kumtetea mhindi mwenye kila dalili ya kutupiga na kumlaani rais wetu anayejitahidi kututetea,,,,.

Napata mashaka na uraia wa watu aina hii.... Pengine wametumwa.
 
Passport ni mali ya serikali na imeandikwa katika page ya kwanza, kwamba inaweza kuchukuliwa wakati wowote.

Raisi wa JMT, au waziri Mkuu au waziri mwenye dhamana wote wanayo mamlaka ya kuagiza/kuamuru passport kuchukuliwa kutoka kwa alie nayo kwa sababu mbalimbali kama vile usalama wa taifa, maslahi ya taifa na matumizi yasiyo mema.

Kwa hiyo, huyo mhindi kuna sababu maalum ya kuchukuliwa passport yake.

Raisi huwa hatoi kauli hadharani kama watu wengine bila kuwa na taarifa zote muhimu.

Wakati mwingine tuwe tunatumia muda kidogo kujifunza mambo madogo na ya msingi kama haya.

ukiamuka utaelewa
 
Umeelewa nilichoandika? Wanachukua kwanza passport yako huku unahojiwa au upo mahabusu au upo nje kwa dhamana lakini lazima wachukue kwanza pass yako. Mwulize Eddo Kumwembe akusimulie.
Nmekuelewa Ila wewe Ndo hujanielewa
wanaichukua ukiwa chini ya ulinzi tear sio Kama hii saga apa bongo ya kunyan'ganywa kienyeji
 
Inashangaza mbongo mwenzangu amekomaa kumtetea mhindi mwenye kila dalili ya kutupiga na kumlaani rais wetu anayejitahidi kututetea,,,,.

Napata mashaka na uraia wa watu aina hii.... Pengine wametumwa.
anakutetea nini?
 
Kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza Mkandarasi wa Maji huko Lindi anyang'anywe pasipoti yake.

Ila kwa upande wangu sioni kama limefuata sheria kwani pasiport ni mali ya nchi iliyompatia mhusika na kwa mujibu wa sheria ya pasipoti, nchi husika huomba raia wake alindwe kwa namna yoyote na host country na ikibidi kukamatwa basi nchi husika ijulishwe. Swali langu, je Mkandarasi huyu kavunja sheria ipi ya nchi?

Kama alichelewa kulipwa fedha za mradi tulitegemea ajenge kwa fedha zake mfukoni?? Naomba kujuzwa kwani elimu yangu ni ndogo.

"Under the law of most countries, passports are government property, and may be limited or revoked at any time, usually on specified grounds, and possibly subject to judicial review"

Atanyang'anya passport hivi anajua wanazo passport ngapi hao jamaa? Sababu anaweza kuwanyang'anya za India akazani amemaliza kazi kumbe bado wanazo kadhaa za nchi za western na wakamtoka vile vile wakiamua.
 
Washauri wa rais wanaweza kuwa wanamshauri rasi vibaya. Matokeo yake Mh.Rais anafanya maamuzi yenye utata yanaweza kwa namna moja au nyingine kuwa kikwazo kwa wawekezaji wa ndani na wakimataifa.
Ushauri mbaya umeanza kuharibu ''brand'' ya nchi yetu na sio jambo la kujivunia Tanzania kuwa branded kama Nchi isiyofuata Utawala wa Sheria

Jambo la msingi hapa ni kwamba nchi inaongozwa utawala wa katiba na sharia. Hata wawekezaji huzingatia sheria zetu zinamlinda au kumfaidisha vipi. Hakuna muwekezaji anayeweza kuwekeza mabilioni ya fedha bila kufahamu vyema sheria za nchi zenye uhusiano na uwekezaji au biashara yake. Sasa ikiwa nchi haifuati sheria na katiba muwekezaji anakuwa hana uhakika wa usalama wake. Kwa hiyo katika kuvutia wawekezaji hatuna budi kufuata utaratibu wa sheria, na kama tunaona kuna mwanya basi vyombo vya kutunga sheria vipi.

Yaani hata tukitaka kuweka sheria ya kunyanganya wawekezaji au wakandarasi passport tunaweza kuweka hiyo official kupitia bunge.

Jana katika vyombo vya habari tuliona tamko la Mh.Rais kwa Mkandarasi wa miundombinu ya maji mkoani Lindi, palepale polisi walichukua hatua ya kumpokonya mkandarasi wa watu passport yake.

Ninapinga kunyanganywa passport kwa mkandarasi huyo. Sipingani na rais maana ninajua rais kabla hajachukua hatua hushauriwa kwanza na wataalam husika. Kwa hiyo napingana na waliomshauri rais.

Sipingi kwa maana ya kumtetea mkandarasi kutokutimiza wajibu wake kwa wakati, la hasha ninapinga kutokufuata taratibu za kumwajibisha mkandarasi.

Serikali iliingia mikataba/mkataba na mkandarsi kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji. Mikataba yetu huingiwa na kutekelezwa kwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya 2011 na Kanuni zake za 2013. Hiyo kuanzia uingiaji wa mkataba, utekelezaji na hata kusitishwa kwa mkataba ni lazima vifanyike kwa mujibu wa vigezo vya mkataba husika sambamba na Sheria ya Manunuzi ya 2011 na Kanuni zake za 2013. Na katika hizo taratibu hakuna taratibu za kunyanganya mkandarasi passport.

Sheria ya Manunuzi ya 2011 na Kanuni zake za 2013 na Mikataba ya miradi mikubwa kama ya miundombinu ya maji imeweka utaratibu mzuri sana wa kumwajibisha mkandarasi anayechelewesha kazi.

Kanuni ya 112 ya Kanuni za Manunuzi ya Umma unasema kuwa ikiwa mkandarasi atachelewa kumaliza kazi kwa mujibu wa mtakaba, atakatwa 0.1% mpaka 0.15% ya thamani ya mkataba wake kwa siku zilizocheleweshwa. Na makato hayo hayatazidi asilimia 10(10%) ya thamani ya mkataba.

Na kama utaendelea kuchelewesha kazi above the limit of liquidated damage, taasisi nunuzi itasitisha mkataba kwa kuwa mkandarasi amekiuka mkataba. Mkataba utasitishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 113 na Mkataba husika. Kama kusitishwa kwa mkataba kutasabibishwa na uzembe wa mkandarasi mitambo na vifaa vyote vitakavyokutwa site zitakuwa mali ya taasisi nunuzi

Hakuna kanuni inayotaka mkandarasi apokonywe passport.

Hii ni kuwatisha wawekezaji hasa wa nje
acha mbwembwe mkuu uyo ananyan'anywa na kazi atamalizia apende asipende we kama unaona Rais hajui kuwa wwe bas umwachie ..tumechoka na kubembelezana utaki pita ivi unataka piga kazi wa LIndi wanahitaji maji si vinginevyo
 
Mambo mengine ni magumu kidogo au ni ya kimwendokasi zaudi. Kimsingi Kuichukua passport ya raia wa kigeni (bila kuripoti kwenye nchi husika kosa la kuzuia passport hiyo tena kwa maelekezo ya hakimu, jaji nk) hakumzuii raia huyo kusafiri. Kwa sababu anaweza kuripoti passport yake imeibiwa tu then nchi yake ikampa passport nyingine. Unless serikali ilioichukua ikatoe taarifa katika consulate ofisi yao. Na hapo tatizo litakalokuja ni where is legal mandate inayomtuhumu mhusika kiasi cha kuzuiwa passport yake (ambayo si mali ya nchi iliyochukua). Mwafaaa!
Tatizo lenu ni kupenda kuzugumzia vitu vidogo vidogo. Mnapaswa kufahamu kuwa Rais ambaye ni Mkuu wa nchi na Serikali ana taarifa zote zinazohusu miradi ya maendeleo, na kama imekwama, anafahamu pia sababu za kukwama kwake. Rais anafanya informed decisions siyo hizo hisia zenu. Be neutral you will get the whole truth.
 
Kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza Mkandarasi wa Maji huko Lindi anyang'anywe pasipoti yake.

Ila kwa upande wangu sioni kama limefuata sheria kwani pasiport ni mali ya nchi iliyompatia mhusika na kwa mujibu wa sheria ya pasipoti, nchi husika huomba raia wake alindwe kwa namna yoyote na host country na ikibidi kukamatwa basi nchi husika ijulishwe. Swali langu, je Mkandarasi huyu kavunja sheria ipi ya nchi?

Kama alichelewa kulipwa fedha za mradi tulitegemea ajenge kwa fedha zake mfukoni?? Naomba kujuzwa kwani elimu yangu ni ndogo.

"Under the law of most countries, passports are government property, and may be limited or revoked at any time, usually on specified grounds, and possibly subject to judicial review"

na kuna taarifa hela alizokuwa analipwa alikuwa anahamishia India kwa mradi mwingine!
 
Siyo mwekezaji ni mkandarasi...
Tutajua baadae kanjbai asituletee utapeli bils zetu kala maji hamna halafu akae na passport aje atukimbie..
Alete maji asituletee mchezo maana hata yeye mkataba unasema atajenga mradi wa maji uishe 1 March 2015 now 2017 maji hollah
Angekuwa amesimama ujenzi na hela stahiki kalipwa wallah nakuhakikishia angewekwa ndani!! Lakini kilichojidhihirisha ni kwamba pesa hakuna(wahisani wamesimamisha) naye akasimama ujenzi kadri ya pesa aliyolipwa!!
Sasa hofu ya kutoroka inatoka wapi!!? Kuna refference yeyote juu yake ya kutoroka labda!? Tulimpaje kazi mtu tuliye na mashaka naye!?
 
Mambo mengine ni magumu kidogo au ni ya kimwendokasi zaudi. Kimsingi Kuichukua passport ya raia wa kigeni (bila kuripoti kwenye nchi husika kosa la kuzuia passport hiyo tena kwa maelekezo ya hakimu, jaji nk) hakumzuii raia huyo kusafiri. Kwa sababu anaweza kuripoti passport yake imeibiwa tu then nchi yake ikampa passport nyingine. Unless serikali ilioichukua ikatoe taarifa katika consulate ofisi yao. Na hapo tatizo litakalokuja ni where is legal mandate inayomtuhumu mhusika kiasi cha kuzuiwa passport yake (ambayo si mali ya nchi iliyochukua). Mwafaaa!
Kwa akili yako unadhani Tanzania gvt haitotoa taarifa kwa serikali husika? Au ulitaka aeleze kila hatua itakayochukuliwa? Serikali inafahamu taratibu zote hizo.
 
Back
Top Bottom