Agizo la Magufuli laibua utata

Angekubali kushaurika yasingemkuta haya ya mdororo wa kiuchumi haijawahi kutokea katika nchi hii! Na sababu hapendi kushaurika wanamuachia limfie! Kuanzia dec mapato yatashuka big time na ndio watakaposhindwa hata kulipa mishahara na elimu bure....wataramba matapishi yao ya matamko ya mihemko yoote anzia bandarini na kwingineko....ile vat lazima itolewe bandari iwe inafanya kazi la sivyo nchi inazama hiii.....
 
Hii ni cheap politics. Kwa mtu asiyejua utawala atakubaliana Na hoja hizi mufilisi. JPM yupo right ni shida sana kuongoza mtu asiyewajibika kwako. Pili hata Account Officer katika taasisi yeyote anaweza kuagiza hayo malipo yakalipwa ila kuna auditor. Auditor akija ndiye Kiboko ya accounting officer hata awe IGP. Refer lugumi case
 
sichangii niko na maumivu ya GEREZANI.

swissme
Kwanza were humu ulipotea
Pili umetoa comment hii

Wewe ni miongoni mwa wale jamaa walionyimwa dhamana na kutopelekwa mahakamani lisu akaingilia kati?
 
Amri yoyote ya ya mkuu ni AMRI HALALI kwa wakati huo! Ndiyo maana polisi wanapoambiwa wamiminie waandamanaji risasi huwa hawana ruhusa ya kuhoji,japo wanajua kuwa katiba inakuhusu maandamano ya Amani! Pia mkuu wa mkoa si askari kicheo,bali ni askari wa ngazi ya juu kabisa kisiasa!! Ndiyo maana ana uwezzo wa kumwamrisha Rpc kufanya chochote! Hata kumweka ndani mtu bila sababu yoyote!
 
Wewe mleta mada ni MWONGO. Ni mmoja ya waathilika wa maamuzi hiyo. Polisi/JWTZ wana wataalam wa kada zote. Wacha waendeshe mambo yao kadiri ya ethics zao. Hoja ya matumizi mabaya ya amri haina mashiko hata kidogo. Naamini kabisa kwa agizo la raisi la kuwaondoa raia kwenye vyombo vya usalama, fedha zitasimamiwa kwa nidhamu kubwa zaidi kuliko kuweka raia ambao hufanya ufisadi mkubwa, na hivyo kuchafua sifa ya majeshi yetu. Utaratibu wa kuweka raia kusimamia fedha kwenye vyombo vya usalama haufai, na hakuna hoja ya msingi kufanya hivyo. Raia wote watoke. Naunga mkono agizo la RAISI JPM. Wafanyakazi raia waliowengi ni mafisadi.Waende wakafanye ufisadi uraiani.
Note: Mimi ni raia wa kawaida,siyo mwanajeshi. Napenda mambo yote ya jeshi yaendeshwe na wanajeshi wenyewe, ili kulinda hadhi ya jeshi. Hawa raia tubaki nao mitaani.
 
mkuu somo la amri pitia kesi ya zombe ndio utalielewa, ina maana wewe hujawahi kuisikia kabisa?
 
Kwanza were humu ulipotea
Pili umetoa comment hii

Wewe ni miongoni mwa wale jamaa walionyimwa dhamana na kutopelekwa mahakamani lisu akaingilia kati?
kuna jamaa huwa anipendi kweli siju ni nini yaa kila yeye akiwa zamu basi ni magereza moja kwa 1.mod 1 2 3 asante ....



swissme
 
we jamaa issue ya lugumi sio ya kawaida, ile sio ya ki odita ilikuwa ya ku mtest mh.
 
Unayosema ni kweli kwamba ingawaje kiutaratibu jeshi linaendeshwa kiamri na aliye chini hawezi kuhoji amri kutoka juu lakini hapa tuwe wakweli pia! Hivyo ulivyosema NDIVYO INATAKIWA KUWA! Hata kama mimi ni Koplo, wewe Major hauna mamlaka ya kijeshi ya kuniamrisha NIKAKULETEE DEMU wako... ukifanya hivyo; maadili ya kijeshi yananipa nguvu ya kukukatalia! Hivyo ndivyo INAVYOTAKIWA! But when we go to the real world... I mean to the real military world, hali ni tofauti! Ni askari wachache sana tena sana wenye ubavu wa kuhoji amri zisizo halali... ni almost HAKUNA! Ni ngumu sana kwa junior officer kuhoji amri isiyo halali ya Brigerdia ingawaje anayo haki hiyo! Ikiwa hata huku uraian watu wanaingia matatizoni kv tu walitii tena shingo upande amri za mabosi raia wenzao, seuze majeshini?!

Lakini tukirudi kwenye mada kuu; Mhasibu Raia ana uwezo wa kutotii amri ya Mheshimiwa mwenye manyota si tu kwa sababu hawajibiki kwenye military chain of command lakini vile vile yeye si mwajiriwa ama wa jeshi au wizara husika ya ulinzi. Hii ndiyo sababu ambayo pia miaka takriban 8 iliyopita wakati serikali inaajiri Internal Auditors; ikaonekana hawa wasiwe waajiri wa halmashauri moja kwa moja bali wa Hazina.
 
Oh! Kwahiyo kumbe haina haja ya kuweka kinga kwavile tiba ipo!!!!
 
Kwahiyo hao askari wao sio mafisadi sio kwa sababu tu ni maaskari?! Labda umemsahau yule Mheshimiwa wa Jeshi la Polisi aliyekutwa na nyumba takribani 40!!!
 
we jamaa issue ya lugumi sio ya kawaida, ile sio ya ki odita ilikuwa ya ku mtest mh.
Nilichotaka kueleza ni kuwa fedha yote ikiingia katika taasisi inayopewa ruzuku na serikali ni ya serikali. PST ndiye mwenye hiyo pesa. Hivyo PST mwisho wa mwaka anatuma maodita kwenda koditi kila kitu na wahasibu na kama kuna mapungufu mhasibu mkuu anasukuma hiyo kasheshe kwa Accounting Officer ambaye anawajibishwa kisawasawa. Hivyo ni hoja mufilisi kufikiria kuwa Mhasibu akiwa ni Polisi ndiye anatapokea amri na kutekeleza (kwa vile ni Polisi). La hasha hata uraiani mhasibu akiambiwa lipa na mwajiri wake analipa ila odita akija kibao kinamgeukia huyo mwajiri. Nadhani umenipata
 
One man show, kama hamkujua kuwa wasukuma wengi wanapenda masifa, ndo mjionee sasa, MWL.Nyerere alishawahi kuonya huko nyuma kuhusu kabila hili kubwa kuongoza nchi, tumekyuka kwa hiyo tusilaum mtu.
 
Una hoji Amri Jeshini???? Mmmmh
 

Aisee kaa utulie kama wewe siyo Mwanajensi na ujawai kukaa na Mwanajensi, ni mafisadi kupita kiasi...siku hizi wana kamsemo kua jensi la siku hizi ni pesa.

Ndugu kuna pesa zinapigwa kula na hao wakuu vya kufa mtu, ila mimi bado najiuliza kwanini haya yanatokea hapa Tanzania?
B. Mkapa katika utawala wake alijivisha waziri wa habari na alifanikiwa sana kwa kuthibiti uhuru wa kutoa na kupata habari na hili alifanikiwa wenda kwa sababu aliwahi kua mwanahabari uko nyuma.

J.M.Kikwete nae akaja akapora Wizara ya mambo ya nje kisa tu alitaka kua maarufu zaidi akasahau majukumu yake kama mkuu wa nchi bali akawa waziri wa mambo ya nje kwa hili alifanikiwa kisa aliwai kudumu kama waziri wa mambo ya nje.

J.P. Magufuli nae naona anajivisha kua waziri wa fedha na mipango na kibaya zaidi amechagua upande wa kuua uchumi wetu sijui kama atafanikiwa make sijaona ni wapi anayo utaalam wa mambo ya fedha na mipango.

Hivi kungekua na uzito gani kama suala nyeti na nzuri kama hili lisingawekwa wazi ili wadau watoe michango yao?
 
Oh! Kwahiyo kumbe haina haja ya kuweka kinga kwavile tiba ipo!!!!
Asikudanganye mtu TIBA ipo ndugu yangu. kuna PAC etc ndo maana utaambiwa fulani katumbuliwa watu wanadhani ameonewa! Utakuta odita akija mhasibu anasema ukweli kwa kuonyesha maandishi kuwa nilimshauri akakataa. Tuache cheap politics za kumzonga JPM. Akikosea tumnange lakini akifanya kweli tumpongeze. Hivi unajua ugomvi wa JPM na ndugu zetu ni nini? Amewabana kimaslahi ndizo hizo chuki zote. Wakati wa JK walivuna kweli hasa akina .... (nakuomba niilishie hapo sitaki BAN mie)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…