BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,782
Agizo la Kikwete kwa Tanesco laiva
Faraja Mgwabati
HabariLeo; Thursday,December 27, 2007 @00:02
MUSWADA ambao utaondoa ukiritimba wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika kutoa huduma ya umeme nchini na kutoa ruhusa kwa kampuni binafsi kutoa huduma hiyo, umekamilika na unatarajiwa kuwasilishwa kwenye kikao cha Bunge lijalo.
Endapo muswada huo utapitishwa na Bunge na kufanywa sheria, kampuni binafsi zitaweza kuzalisha na kusambaza umeme zenyewe bila kuiuzia Tanesco kama ilivyo sasa; kitu ambacho wataalamu wamesema kitapunguza bei ya nishati hiyo muhimu. Akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kutimiza miaka miwili madarakani, Ijumaa iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alielezea nia ya serikali kubadili sheria inayoipa nguvu Tanesco ya kuhodhi mamlaka ya kutoa huduma hiyo.
Akizungumza na HabariLeo jana, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alisema maandalizi ya muswada huo yamekamilika na kilichobaki ni kuupeleka bungeni kwenye kikao kinachotarajiwa kuanza Januari 29, mwakani. Karamagi alisema endapo muswada huo utapitishwa na kisha sheria kuundwa, kampuni binafsi zitaisaidia Tanesco katika kutoa huduma ya umeme ambayo yanakua kila siku.
Alisema pamoja na Tanesco kufanyia ukarabati mitambo ya kusambaza umeme waliyonayo, haitaweza kukidhi mahitaji, hivyo kuibuka kwa kampuni nyingine kutasaidia kutoa huduma nzuri. Unajua ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndiyo wanapata umeme, kwa hiyo mahitaji ya umeme bado ni makubwa, alisema Karamagi alipoulizwa kama kuingia kwa kampuni binafsi hakutawanyanganya wateja Tanesco.
Kuhusu kama hatua hiyo itasaidia kupunguza bei ya umeme, Karamagi alisema bei itapungua kwa sababu Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), itadhibiti huduma hiyo kwa muda hadi hapo ushindani utakapokuwa wa halali kati ya kampuni zitakazokuwapo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Artumas, ambayo hujihusisha na utafutaji wa mafuta na gesi nchini, Salvator Ntomola, alisema hatua hiyo ni nzuri kwa sababu itawapa unafuu wa bei wananchi kutokana na kuwapo kwa ushindani katika huduma hiyo muhimu. Ntomola alisema kwa sababu wazalishaji na wasambazaji watakuwa wengi, kutakuwa na ushindani kama ilivyotokea kwenye kampuni za simu za mikononi, ambapo kuingia kwa kampuni binafsi kumeboresha huduma na bei ukilinganisha kabla ya hapo.
Tukiwa wengi ndiyo vizuri, Ewura itafanya kazi vizuri ya kudhibiti bei na utoaji wa huduma, alisema Ntomola. Aliungana na Waziri Karamagi kwamba Tanesco haitaathirika endapo kampuni nyingine zitaingia kwenye biashara hiyo, akisema Tanesco imeshajijenga na ina miundombinu mingi kuliko kampuni binafsi.
Tanesco bado itakuwa na nafasi ya kufanya vizuri kama ilivyo kwenye kampuni za simu, TTCL ina advantage (unafuu) kuliko kampuni nyingine za simu za mkononi, alisema. Hatua ya kuruhusu soko huria kwenye umeme inakuja wakati ambao Tanesco imeiomba Ewura kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 40 ili kukidhi mahitaji ya kifedha kwa ajili ya kumudu gharama za uendeshaji.
Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved