Habari zenu wana JF
Basi bila ya kupoteza muda niingie kwenye mada kamili.
Ilikuwa jana katika harakati za kusakata kabumbu, baada ya maandalizi mazuri kabla ya mchezo kukamilika, tukaanza rasmi mchezo. Uwanja ulikuwa umeloa sana hivyo nyasi zikawa zinaruhusu vizuri pasi na mashuti kufika eneo husika kwa uzuri.
Katikati ya mchezo muda ambao mechi imekolea pande zote mbili, ghafla filimbi ikaanza kusikika, pree, pree, pree, pree, pree, kwa kila shuti ambalo lilikuwa linaelekezwa golini. Mara nikaona mood ya golikipa imeanza kubadilika na hapo hapo akadai amechoka, mara anajisikia vibaya.
Nilijaribu kumbembeleza golikipa kuendelea lakini aligoma kuendelea na mchezo na kibaya zaidi nilikuwa bado sijafunga goli. Hapa mastraika ndio tunaelewa uchungu wa kwenda kucheza mpira halafu usifunge goli hata moja, huwa inauma sana.