Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,181
- 3,215
Mbunge wa Siha na Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa, Aggrey Mwanri amekuwa na tabia mbaya sana kwa wananchi wake, hasa kwa wananchi wanaomzunguka kijijini kwake.
Kiongozi huyu amefanikiwa kununua mashamba ya majirani wanaomzunguka, kwa kuwa jirani zake ni masikini na wasio na elimu ya kutosha, Mbunge huyu kwa kutumia uwezo wake wa kifedha amekuwa akiwashawishi majirani zake maskini wamuuzie mashamba yao. Kwa kuwa wananchi hao ni masikini, ukubali kuuza mashamba hayo kwa Mbunge wao. Hivi sasa Mbunge huyu anamiliki maeneo makubwa kata ya WANDRI wilayani Siha.
Aina ya uongozi wa hivi ni hatari, badala ya kiongozi kuwasaidia wananchi wake ili watumie mashamba yao kuwakwamua ki uchumi, yeye amegeuka kuwa mnunuzi wa hayo mashamba, hii inasikitisha sana hasa ukifika kijiji anachotokea Mheshimiwa huyu. Unapomshawishi mwananchi asie na uwezo akuuzie ardhi, huu ni utapeli kama itapeli. Hii ni tabia mbaya kwa viongozi