Agenda kuu: Tunataka Tume Huru Ya Uchaguzi

GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,038
2,000
Tume ya uchaguzi ya sasa haina sifa hata ya kusimamia uchaguzi wa mtaa au kitongoji.

Tunataka tume huru ya uchaguzi itakayoweza kusimamia,kuheshimu na kulinda sheria za uchaguzi.

Sio muda wa vyama vya upinzani kuibembeleza tume ambayo imeshaonyesha jeuri na kiburi wala haiwezi kuheshimu na kulinda sheria za uchaguzi.

Mnaibembeleza tume ya uchaguzi ambayo imewekwa mfukoni na mwenyekiti wa chama tawala cha siasa ambacho na chenyewe ni miongoni mwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi?

Mnaibembeleza tume ambayo inaruhusu askari kuingia ndani ya chumba cha kupigia kura kinyume na sheria kisha kukamata mawakala wa upinzani na kuwaweka kizuizini?

Mnaibembeleza tume ya uchaguzi ambayo DC,RC,RPC anaingia chumba cha kupigia kura/kujumlisha kura kinyume na sheria kwa mitutu na kuamuru mgombea wa chama tawala atangazwe mshindi hata kama hajashinda?

Mnaibembeleza tume ambayo imeruhusu mawakala na wafuasi wa vyama vya upinzani kupigwa,kuumizwa na kuteswa kwa zana mbalimbali?

Mnaibembeleza tume ya uchaguzi ambayo mwenyekiti wa tume,mkurugenzi wa tume ya uchaguzi,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wanateuliwa na mwenyekiti wa chama tawala ambacho nacho kinashiriki uchaguzi?Na anayewateuwa anawaagiza kuwa ole wenu mkawatangaze wapinzani bado mnawabembeleza hao tume?I you serious?

Ndugu zetu malawi hawana tume huru ya uchaguzi lakini tume yao imekaa kama ifuatavyo.

1.Kila chama kinachoshiriki uchaguzi kinawakilisha wajumbe wawili tume ya uchaguzi.

2.Mashirika yasiyo ya kiserikali NGO'S yanawasilisha majina ya wajumbe wawili wa tume ya uchaguzi.

3.Tume ya uchaguzi ni lazima pia iwe na wajumbe wawakilishi wa dini.

4.Mkurugenzi wa uchaguzi anateuliwa na Rais lakini mpaka bunge lilidhie na kumpigia kura za ndiyo.Wabunge wakipiga kura za hapana Rais analazimika kuteuwa mtu mwingine.

5.Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anateuliwa na Rais na kisha jina lake hupelekwa bungeni linajadiliwa na wabunge kisha kupiga kura za ndiyo wabunge wakipiga kura za hapana Rais analazimika kuteuwa mtu mwingine ambaye bunge litamridhia..Na ndio maana mama joyce banda alivyoshindwa uchaguzi 2014 alitangaza kufuta uchaguzi mwenyekiti wa tume akamjibu kuwa Rais hana mamlaka ya kutengua uchaguzi.Hii ndio Malawi electoral commission tume ya uchaguzi ya malawi.

Leo sisi tuna tume Mwenyekiti wa tume na watumishi wote wa tume mpaka mwenyekiti wa tume wanateuliwa na Mwenyekiti wa chama tawala ambacho na chenyewe ni mdau wa uchaguzi..Unategemea kwamba Rais akishindwa uchaguzi akifuta huo uchaguzi mwenyekiti wa tume anaweza kuwa na ujasiri wa kumuambia Rais kuwa hana mamlaka?

Mamilion ya wananchi wamekata tamaa ya kupiga kura kutokana na tume mbovu ya uchaguzi kata yenye wapiga kura elfu 12 wanapiga kura watu elfu 1 bado mnataka mazungumzo na tume iliyokosa sifa ya kusimamia uchaguzi?Tume iliyosababisha watu kukosa imani na uchaguzi?

Naunga mkono kususia uchaguzi lakini ni muda wa vyama vya upinzani kupaza sauti,kupambana kwa kila hali,akili na uwezo kudai tume huru ya uchaguzi hata kama itatu-cost maisha yetu.

Nawaambieni ili tuheshimiane tuelekeze nguvu zetu,akili zetu,fedha zetu,uwezo wetu kudai tume huru ya uchaguzi
Tume huru ya uchaguzi uwe wimbo wa wapinzani kususa uchaguzi bila kuchukua hatua stahiki za kufanya tuheshimiane ndani ya taifa hili haitatusaidia,.Tususe uchaguzi na tuanze kazi ya kudai tume huru ya uchaguzi.

By;
Mdude nyagali
Sumu ya nyigu
 

Mwenekaya Nkulu

Senior Member
Jul 16, 2014
142
250
Umenena vyema sana, viongozi wa ukawa inawezekana kabisa kwamba hawana nia thabiti ya kuondoa utawala mbovu uliopo madarakani badala yake nao huenda ni mawakala wa serikali wanaoratibu zoezi la kupunguza (neutralize) hasira za wananchi dhidi ya Serikali kwa kujifanya ni waungwana wakati huo huo wao wanakula kwa mlango wa nyuma
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,568
2,000
Susieni na ruzuku kupinga tume hiyo iliousimamia uchaguzi uliowapa hiyo ruzuku
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom