Agenda gani zipewe kipaumbele 2013?

Agenda gani zipewe kipaumbele 2013?

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Posts
2,492
Reaction score
1,243
Leo ni siku mbili kabla ya kufikia mwaka 2013 mwaka unaotakiwa kuwa mwaka wa kuweka msingi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na ule uchaguzi mkuu wa mwaka 2014. Kwa kawaida nchini mwetu wanasiasa ndiyo huleta Agenda kwa wananchi na siyo wananchi wanaweka Agenda za kufuatwa na wanasiasa. Mwaka 2013 nil lazima watanzania tuweke agenda na wanasiasa wazifuate Agenda zetu!! Kwa mfano naorodhesha mambo machache katika mfumo wa maswali ili kutusadia kama tunadhani wanasiasa wetu wanayo majibu yake.

  1. Tunataka mfumo wetu wa elimu uweje kuelekea Tanzania yenye Katiba Mpya?
  2. Programu za Kilimo ziboreshwe au zifutwe na kuletwa nyingine kwa kuwa zilizopo hazijatuletea tija?
  3. Tufuate Rasmi mfumo upi wa kiuchumi Kiliberali, Kibepari, Kishoshalisti au turudi kwenye siasa ya ujamaa?
  4. Mfumo wa mgawanyo wa Rasirimali zetu ubadilishwe au huu uliopo uendelee?
  5. Sera yetu ya mambo ya nje kuelekea Afrika ya Mashariki na Umajumui wa Afrika iweje?
  6. sheria ya vyama vya siasa iruhusu kuungana kwa vyama

Sisi kama wananchi tunapaswa kuwauliza wanasiasa wetu ni nini misimamo yao mbalimbali kuhusu masuala ya kitaifa na kimataifa, badala ya kuishia kushangilia na mipasho yao ya majukwaani bila ya kujua wanasiamamia nini. Wewe unadhani Agenda Kuu mwaka 2013 iwe ni nini?
 
Back
Top Bottom