Camo
Member
- Jul 15, 2025
- 11
- 70
Kuna ukweli ambao hautasomwa kwenye vitabu vya elite, hautaandikwa kwenye mitandao ya kifeminist au kwenye mafunzo ya “modern relationships.” Ukweli huu hujificha nyuma ya tabasamu la mwanzo, ule wakati wa mapenzi ya ujinga, pale kila kitu kinaonekana rahisi, kila kosa linaweza kufichwa kwa kicheko na kila maombi ya upuuzi yanajibiwa kwa uvumilivu. Hii ndiyo stage ya kwanza — the foolish stage. Ni dunia ya maigizo, ambapo mwanaume anaacha akili yake nyuma ya mlango ili amwingize mwanamke kwenye anga lake. Ni pale ambapo anaacha simu yake mezani kwa makusudi, akificha siri si kwa kuifunga, bali kwa kuikabidhi. Huu ni mtego wa kifahari, si upumbavu wa kweli. Ni jaribio la kumshawishi mwanamke kwamba himaya ni salama, kwamba milango ya siri imefunguliwa.
Lakini hakuna mfalme aliyejengwa kwa siri za WhatsApp. Mwanaume hatabaki kwenye stage hii kwa muda mrefu. Mara zote, kutakuwa na mwamko wa pili — the stage of reality. Hapa ndipo jela ya hila huanguka, na kiti cha enzi kinawekwa katikati ya chumba. Hapa ndipo mwanaume huacha kuvaa mask ya mvumilivu na kuanza kudai heshima ya kweli. Si heshima ya hila, bali ya ufalme. Atataka mwanamke afikirie, sio acheke tu. Atataka chakula kiwe mezani kabla hajaomba, sio baada ya malalamiko. Atataka ukimya wakati akili inahitaji kupumzika, sio maswali ya kitoto pale ambapo mzigo wa dunia unambana mabegani.
Na sasa, changamoto ya dunia ya kisasa ni hii: wanawake wengi wamefundishwa na modern gospel ya televisheni, Twitter na vitabu vya kisasa kwamba stage ya kwanza ndiyo mapenzi yenyewe. Wameaminishwa kwamba mwanaume wa kweli atabaki “mnyenyekevu” na “mwenzako” katika foolish stage milele. Wamekataa mwaliko wa kuingia katika stage ya pili — pale ambapo akili, busara, na nidhamu zinahitajika. Ndiyo maana wanaishia kero, wakionekana kama mizigo.
Huu ndiyo msalaba ambao jamii ya kisasa imeubeba kwa makusudi. Tumeunda kizazi cha wanawake wanaopenda burudani ya mwanzo lakini wanakimbia ukali wa uhalisia. Wamefunzwa kukaa katika starehe ya kubembeleza na kukataa shinikizo la kutumia akili. Wanadhani mapenzi ni mchezo wa kuendeleza foolish stage, wakati mapenzi ya kweli ni ukuta wa kutumikiana kwa heshima na akili.