Afya yatumia bilioni 1/- pasipo idhini ya Bunge

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetumia Sh. bilioni 1.01 kwa ajili ya maonyesho ya kilimo maarufu kama Nane Nane katika mwaka wa fedha 2009/2010 ambazo hazikuidhinishwa na Bunge.

Kwa mujibu wa majibu ya Serikali kuhusu taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kwa Hesabu zinazoishia Juni 30, mwaka 2010, ilibainika kuwepo kwa matumizi ambayo hayakuwemo katika bajeti iliyopitishwa na Bunge.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), ilitoa mfano wa serikali kutumia fedha nyingi katika kuratibu shughuli za maonyesho ya kitaifa ya Saba Saba, Nane Nane na Utumishi.

Ilisema katika kupitia hesabu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kamati ilibaini kuwa kwa mwaka 2009/10, wizara ilitumia fedha za matumizi ya kawaida Sh. bilioni 1.101 kwa ajili ya kuratibu shughuli za maonyesho ya Nane Nane na ujenzi wa jengo la Nane Nane.

Ikijibu hoja hiyo, Serikali ilisema imetoa maelekezo hayo kwa wizara zote kushiriki maonyesho ya Nane Nane kwa nia nzuri kabisa kwa lengo ya kuzipa nafasi wizara, idara na taasisi fursa kuwaonyesha wananchi shughuli zinazofanywa.

Serikali ilisema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ilitumia Sh. bilioni 1.01 kugharimia maonyesho hayo na kubainisha matumizi kuwa Sh. milioni 729 zilitumika kama posho, dawa, mahema na chakula.

Aidha, ilisema Sh. milioni 372 zilitumika kujenga majengo ya Nane Nane na kwamba jumla ya watumishi 350 walishiriki maonyesho hayo.

Ilisema wagonjwa 30,139 walipatiwa huduma mbalimbali za afya ikiwa ni pamoja na kutibiwa na kupata ushauri wa kitaalam.

Hata hivyo, ilisema serikali itazingatia maelekezo na ushauri uliotolewa wa kupunguza matumizi katika maonyesho mbalimbali yatakayoandaliwa baadaye.




CHANZO: NIPASHE

 
1bil for exhibition, 0.5bil ya ukarabati wa nyumba MOJA ya aliyekuwa w/afya Dk.Haji Mponda kule Dodoma...halafu mahospitalini hakuna vitanda, madawa wala vifaa na waTZ tumeridhika!!!!
 
Walikuwa na ruksa ya ikulu hivyo hawajakosea. Bunge lingekuwa na meno na viwango wahusika wangeshughulikiwa. Lakini bunge lenye spika kihiyo kama Makinda unategemea nini?
 
Lakini mbona hamsemi magambaz wanaiba mabilioni kila mwaka bila ya idhini ya Bunge?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom