Afya ya Mugabe inazidi kuzorota!

Waganda walikuwa wanagwaya sana kwa maswali haya. Sasa niulize hivi; Ni kweli Wazimbabwe na kusoma na 'kuendelea" kwao wanaona kwamba bila Mugabe Zimbabwe haiwezekani? Kweli?

Heshima kwako Bysel,

Mkuu naomba kujibu swali lako kwa kukuliza swali.

Unaamini utawala wa Mugabe umewekwa kwa ridhaa ya wananchi wengi wa Zimbabwe?.Ikiwa jibu ni hapana basi hawastahili kulaumiwa kwa kuongozwa na kiongozi mzee aliyepitwa na wakati.Ikiwa jibu ni ndiyo kabla ya kutoa lawama kwa wazimbabwe yatupasa tujitazame sisi watanzania kwa kumchagua Rais mgonjwa anayeanguka majukwaani kila mara.Jiulize hakuna mtanzania mwingine mwenye afya nzuri anaeweza kushika wadhifa wa urais ?.

Mkuu system[katiba] za nchi za kiafrika nikichefu chefu.
 
Robert Mugabe anapenda sana kuishi maisha ya fahari na kutawala. Anapenda afe akiwa Rais halafu ahudhurie na mazishi yake ambayo yatakuwa ya kifahari.
 
Back
Top Bottom