Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,790
Habari za leo wapendwa,
Leo hii nimeona tuongelee afya za akili, wengi wetu tunashindwa kuelewa afya ya akili ni kama afya fisikia ya mwili, na inatibika kitaalamu. Katika jamii yetu tunaamini mtu akishaugua kichaa hawezi kupona kabisa, wengine matatizo yao ya kichaa katika familia wanaogopa kuyapeleka hospitali kwenye msaada wa kitaamu wakiamini jamii ita wa label, na kuwa stigma zed, wengine hu hofia pia watoto wao kukosa wachumba watu wakigundua kuwa ukoo ule una asili ya kichaa.
Kuna bwana mmoja ninaemfahamu, mke wake alipatwa na matatizo ya ugonjwa wa akili, yule dada ghafla aliacha ucheshi, alikuwa mtu wa kukaa kimya tu. Mume aliona ni kero nyumbani akawa akitoka kazini anakwenda kupiga bia kwanza kuliko kuwahi nyumbani utazamane na zombie.
Siku aliyorudi nyumbani na kukuta suruali zake zote zimekatwa baba aliomba ndugu wa mke wamchukue mtoto wao ndoa yeye imemshinda. Ndugu wa mke walimpeleka ndugu yao Muhimbili, yalikuwa matibabu ya muda mrefu, lakini yule dada alipona na akawa anaendelea na maisha yake, lakini hakutaka tena kurudi kwa mume wake.
Kama yule bwana angekuwa na ufahamu wa kuwa alitakiwa ampeleke mke wake kwenye matatibabu ndoa isingevunjika.