AFYA MUHIMU SANA WANAUME SOMA itakusaidia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AFYA MUHIMU SANA WANAUME SOMA itakusaidia

Discussion in 'JF Doctor' started by aloveragel, May 3, 2012.

 1. aloveragel

  aloveragel Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AFYA YAWABABA!
  “Wanaume tujue Prostate yetu”.
  Kwa nini tujue?
  l “Kufahamu Ugonjwa kutasaidia kujizuia”
  l “Kujua ugonjwa ni NUSU ya Tiba”
  Tezi la Prostate: Ni tezi la mfumo wa uzazi wa mwanaume iliyopo
  chini ya mfuko wa mkojo (BLADDER).
  Nani ana Prostate?
  – MWANAUME
  – ¨ Prostate IPO wapi?
  – Chini ya kifuko cha mkojo
  – Imeizunguka URETHRA (mrija unaounganisha bladder and
  uume) humsaidia mwanaume kukojoa.
  Testosterone na kuvimbaprostate(BHP)
  l Testosterone – Ni Homoni za uzazi za mwanaume.
  l Ni muhimu kwa maumbile ya mwanaume: URIJALI, Misuli
  imara.
  Mwanaume anapofika miaka 40 na zaidi mimeng’enyo ya Prolactin
  inayozalisha testosterone inayozalisha dihydrotestosterone
  inaongezeka
  MATOKEO:
  Nywele kupungua, KUVIMBA kwa tezi la prostate BHP. Hii
  husababisha kubanwa kwa urethra na kusababisha mkojo kushindwa
  kutoka nakushindwa kwa tendo la ndoa.
  Dalili za kuvimba kwa tezi ya prostate
  CHOONI
  l Kutaka kwenda haja ndogo mara nyingi hasa usiku.
  l Maumivu wakati wa kukojoa
  l Kasi ya mkojo hupungua kuliko kawaida au una kwama kwama
  l Kushindwa kukojoa
  l Maumivu au hali ya kuungua wakati wa kukojoa
  l Mkojo kuwa na damu
  l Maumivu kwenye kiuno, nyonga na juu ya mapaja
  KITANDANI
  l Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa
  l Maumivu unapofikia kilele
  l Uhanisi
  l Maumivu wakati wa kufanya tendo
  Shida nyingine zinazoletwa na BHP
  l Ugonjwa katika kibofu
  l Ugonjwa wa urethra na figo
  l Mkojo kubaki katika damu (hii ni sumu na ni hali ya HATARI).PROSTATE CANCER: MATOKEO YA UTAFITI
  50%ya wanaume wenye miaka 40-50 na 70% ya wanaume wenye
  miaka 60 wamevimba tezi la prostate. Hata wenye miaka 30,25%
  wana seli za prostate cancer katika miili yao,Seli hizi za cancer ya
  prostate hupatikana kwa wanaume wenye umri kati ya miaka 70,80 na
  kuendelea.
  A-D Staging System
  Hatua A. KANSA
  inaanza.Kiuvimbe kidogo
  ndani ya tezi hakiwezi
  kutambuliwa hata kwa
  kipimo cha DRE.
  Hatua B. Kiuvimbe ndani ya
  tezi kinaweza kutabuliwa na
  DRE.
  Hatua C. Kansa imekomaa.
  Kansa imeanza kusambaa nje
  ya tezi la prostate lakini
  hajafikia viungo vingine.
  Inatambuliwa na kipimo DRE.\Hatua D. Kansa imesambaa
  katika viungo vya karibu na vya
  mbali kama mifupa, nyonga na
  mitoki.
  Vipimo vinavyotumika
  l P. S. A. – Prostate Specific Antigen Test. Hupima damu na kiasi
  cha protini katika seli za prostate kawaida ni ndogo zaidi ya 4 ,
  hakuna uwezekano wa kansa. Kati ya 4 na 22 uwezekano wa
  kansa upo, zaidi 22 uwezekano wa kansa ni mkubwa sana.
  l Kasi ya mkojo – hupimwa ml/sek. Kasi ya kawaida ni 10 na
  32ml/sek.
  l Kidole hupitishwa kwenye njia ya haja kubwa, kuweza kupima
  ukubwa wa prostate.
  Tiba zinazo chaguliwa
  l madawa: inakubaliwa na madaktari wa orthodox.
  Tafiti zinaonyesha:
  l Maelfu ya wanaume wanalio na kansa ya prostate wanapata
  upasuaji usio wa lazima na wengine wanatibiwa na madawa
  yenye sumu yaliyopitwa na wakati kwa sababu ya ujinga wa
  kitabibu??. (Lois Rogers, Medical Correspondent, Sunday
  Times, 27 April1997).
  l moja ya madawa wanayopewa, iligunduliwa miaka 30 iliyopita
  inaharibu Ini, inaleta magonjwa ya moyo,kiharusi na maziwa
  kuvimba na imepigwa marufuku nchi za Ulaya. (Johnathon
  Waxman, Cancer Specialist, Hammer Smith Hospital, London).“Madawa mengi yanayotumika kutibu BPH hayana manufaa sana,
  Yana madhara mengi, yanafanya kazi taratibu, yanaondoa dalili na
  madhara mengi , ikiwamo kupoteza hamu na kuua uwezo wa tendo la
  ndoa”.
  l KISU (UPASUAJI) – hukubaliwa na madaktari wa orthodox.
  l 70% ya wagonjwa wanakua ******* baada ya upasuaji, na 40%
  hawawezi kuudhibiti mkojo (Jonathon Waxman).
  l Njia ya Asili – kuzuia na kutibu.
  l Madaktari wengi wameamini wanaweza kuzuia tezi iliyovimba
  kwa kumpa mgonjwa virutubisho ambavyo amevikosa.
  Matokeo ya tafiti
  l maumivu na matatizo ya prostate yanaweza yakaondosha na
  matumizi ya virutubisho. Hata wale walio na tezi iliyovimba
  hupata nafuu ya haraka wakipewa tiba ya virutubisho (Dr. James
  Balch, Specialist Urology)
  l Tafiti zinaonyesha dhahiri kwamba madawa hayana manufaa
  katika kutibu tezi iliyovimba utaratibu wa kulisha kiungo
  virutubisho vinavyokosekana kutokana na ulaji mbaya au umri
  ndio muafaka katika kurudisha uvimbe (Dr. Hans Kuglor, author
  of the top-selling book, Slowing Down the Aging Process).​
  Katika njia zote hizi ni ipi uionayo ni salama kwako na kwa familia yako?
  wadau tutaendelea na njia ya kuzuia nisiwachoshe sana kama mtapenda niendelee naomba mnijuze
   
 2. k

  ksalama0 Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimeipenda hiyo habari sana kwa manufaa ya afya zetu ktk maisha ya kila siku. Ahsante sana.
   
 3. aloveragel

  aloveragel Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tutaendelea kujuzana kama kukiwa na mda ucjali mkuu
   
 4. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Kazi nzuri, ni jambo jema kukumbuka sana afya zetu kwani ndio teketi yetu ya kuishi duniani!Nategmea mengi toka kwako mkuu
   
 5. aloveragel

  aloveragel Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poa chief mp
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Asante kwa somo. Usitubague, ukimuelimisha mwanamama umeelimisha jamii. Ntaanza kuchungulia mtu akisusuu!
   
 7. REX

  REX JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Aloevera gel,are you a champion? Thats a nyc work.lets stay in touch.
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mkuu asante sana maana shule si darasani hata hapa ninaimani watafaidi wengi sana
   
Loading...