Afya leo: Ubuyu na faida zake

Afya leo: Ubuyu na faida zake

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,841
Reaction score
8,593
Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu.Kila mti au mmea una makusudio yake.
Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi,vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya mwanadamu.Unga wa ubuyu una vitamini na madini mengi kuliko matunda yeyote unayoyajua.

FAIDA ZA UBUYU NA UNGA WAKE

1.Unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.(HUONGEZA KINGA YA MWILI HASA KWA WENZETU AMBAO KINGA IKO CHINI)

2.Ubuyu una kiwango kingi cha kalisiamu(Calcium)mara mbili zaidi ya maziwa ya ng'ombe,pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja madini ya chuma.(HUSAIDIA KUIMARISHA MIFUPA NA MISURI & KUKATA TUMBO-VITAMBI)

3.Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini(HASA WENYE MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME NA KIKE).

4.Ina virutubisho vya kulinda mwili

5.Ubuyu una vitamini B2 & B3 ambayo ni muhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng'enyaji wa madini ya chuma ,kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili wa binadamu huwa na vitamini B2(HII NI NZURI KWA WALEVI WA SIGARA,POMBE)

6.Huongeza nuru ya macho

7.Unga wa ubuyu(juisi)una magnesium ambayo husaidia kujenga mifupa na meno.

8.Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika .

9.Husaidia sana wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo.

JE,UNAPASWA UNYWE KIASI GANI?

*Kunywa kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na muda wa siku kadhaa utaona matokeo ya mwili wako.

NIPENDE KUTAHADHARISHA KWAMBA UNAPOKUNYWA JUISI YA HII NZURI YA UBUYU JIZUIE KABISA USINYWE POMBE NA UVUTAJI WA SIGARA ILI HUIMARISHE MISULI YAKO KWA MAANA NI TIBA.

Wanaume wengi kwasababu ya kukosa nguvu za kiume wamekuwa wakinywa pombe kali(konyagi)ili kuleta msisimko wa kujamiiana na mwenzi wake,hii ni hatari kwa mwanaume.
 

Attachments

  • jifunzekupika-1540825512774.jpeg
    jifunzekupika-1540825512774.jpeg
    54.8 KB · Views: 323
OK asante kwa somo, vitu vya asili/vyakula vilivyo dharauliwa vina maana na umuhimu sana ktk mwili wa Binadamu.
 
natafuta wateja wa juice hiyo waliopo dar wanaoweza kumudu kuagiza lita tano angalau kwa wiki lita moja itauzwa 2500/-.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom