Afya bora ya meno itakuepusha na maumivu ya mara kwa mara ya meno pia harufu mbaya mdomoni

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
1061604

1061607


1061608

1061609

Meno ni muhimu kwa muonekano na sura nzuri. Memo hutusaidia katika kuongea na kuwa na mawasiliano ya kueleweka. Kikubwa zaidi meno ni muhimu katika mfumo wa chakula.

Afya ya kinywa na meno isipozingatiwa, kinywa hutoa harufu, unajikuta hupati mpenzi unadhani umerogwa kumbe unakimbiwa kwa harufu mbaya pamoja na mahela uliyonayo au chura uliyobeba.

Ulimi kwa umbile lake hubakisha mabaki ya chakula. Hivyo baada ya kusafisha meno, ni muhimu kusugua ulimi.

Ni muhimu kutumia dawa yenye floride, madini haya ni muhimu katika kuimarisha meno. Kusafisha meno asubuhi unapoamka na jioni kabla hujalala ni muhimu lakini ukiweza kusafisha kila baada ya kula ni bonus.

Wengi hawasukutui baada ya kusafisha meno ili kuiacha dawa iendelee kufanya kazi.

Watoto tunaweza kuwaanzishia usafi wa meno kuanzia jino la kwanza linapotoka.

Kumbuka kumuona dentist kila baada ya miezi sita.
 
wadada wengine hunuka mdomo sababu usiku kucha amekesha na maiki ana rap, asubuhi hata atumie omo na magadi lazima mdomo uwe mchafu
 
Kuna watu wananuka mdomo mkuu ni balaa, kama umetoka kula ukiongeae nae unaweza kurudisha change.
hahaha sky ,serious ?
ila tz suala la usafi na ustaarabu bado sana,kuna mzee alikua roommate wangu chuoni alikua na viatu vinanuka balaa,afu akitoka chuuo haogi anakaa na jasho chumba kinanuka,chooni haflush kwa kuvuta kamba yeye anamwaga maji kidogo mzigo unaelea.it was disgusing
 
Hivi huwa ikoje unakuta Kuna familia haijawahi sumbuliwa kabisa na ishu za meno?
Tena unakuta ndo zile familia hata uwezo au elimu ya kupiga mswaki Mara ngapi huko hawaijui kabisa?
 
mimi meno yangu yamepasuka na hii inatokea nikiwa mjamzito.. sijui tatizo ni nini


wakati nakuwa walikuwa wakichemsha majimbi au viazi vitamu wanaweka magadi, hivyohivyo maharage na mahindi.. huwa najiuliza ndio maana leo napasuka meno au vipi Sky Eclat
 
mimi meno yangu yamepasuka na hii inatokea nikiwa mjamzito.. sijui tatizo ni nini


wakati nakuwa walikuwa wakichemsha majimbi au viazi vitamu wanaweka magadi, hivyohivyo maharage na mahindi.. huwa najiuliza ndio maana leo napasuka meno au vipi Sky Eclat
Ukiwa mjamzito mnagawana calcium na mtoto. Unahitaji kunywa maziwa kwa wingi.
 
Nooooooooo
Kama huna lililotoboka jitahidi kupiga mswaki pande zote za meno vizuri kisha toa ulimi nje na uupitishe pia mswaki vizuri mambo yatakaa poa.

Pia jitahidi nenda kwa wataalamu wa meno wakuangalie kwa kutumia kioo kwa kupisha pande zote za kinywa unaweza kuwa na jino limetoboka pembeni kwa kuangalia kawaida huwezi ona likawa linabakiza mabaki ya chakula
 
Back
Top Bottom