Afungwa miaka 45 kwa unyang'anyi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429
pic+jela.jpg

Dar es Salaam.
Dereva taksi, Rashid Yusuph(23) amehukumiwa kifungo cha miaka 45 jela, baada ya kupatikana na hatia ya unyang'anyi wa kutumia nguvu.

Yusuph ambaye ni mkazi wa Kimara Mbezi amehukumiwa kifungo hicho jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya hukumu.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia nguvu dhidi ya raia watatu wa kigeni ambao walikuja nchini kwa ajili ya kufanya utafiti na utalii wakitokea nchini Zambia.

Pia, Mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Ramadhani Kingazi (23) ambaye ni mjomba wa mshtakiwa wa kwanza, baada ya kushindwa kumtia hatiani.

Akisoma huku hiyo, hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Ritha Tarimo alisema imemtia hatiani mshtakiwa kama alivyoshtakiwa hivyo atatumikia kifungo cha miaka 45 jela ili iwe fundisho.

Hakimu Tarimo alisema ameridishwa na ushahidi wa mashahidi saba waliotoa mahakamani hapo dhidi ya mshtakiwa huyo.

"Nakuhukumu kifungo cha miaka 45 jela kwa makosa yote matatu ya unyang'anyi wa kutumia nguvu, kwa sababu tukio hili lilitokea sehemu moja na kwa wakati mmoja hivyo, kila kosa moja utatumikia kifungo cha miaka 15 na adhabu hii ina kwenda kwa pamoja," alisema Hakimu Tarimo.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Ashura Mzava aliomba mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo kwani tukio hilo lilifanyika kwa raia wa Marekani ambao wanawakilisha nchi yao hapa nchini.

"Mheshimiwa Hakimu naomba mahakama yako itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa mtu yeyote mwenye nia ya kuharibu taswira ya nchi na kwa yoyote anayefikiria kuibia raia wa Tanzania na wasio kuwa raia wa Tanzania ," alisema Mzava.

Katika hati ya mashtaka, mshtakiwa anadai kutenda kosa hilo Aprili 28, 2016 katika Stesheni ya Tazara iliyopo Wilaya ya Ilala.

Ilidaiwa katika shtaka la pili mshtakiwa aliiba fedha za Zambia kwacha 50, dola za kimarekani 200, kadi moja ya Atm pamoja na saa ya mkononi, mali ya raia wa kigeni, Mariah Melena.

Katika shtaka la tatu, siku na eneo hilo hilo mshtakiwa aliiba dola za kimarekani 250, fedha taslimu Sh 50,000, fedha za Zambia Kwacha 300, simu moja, Ipad, chaji pamoja na flashi mali ya raia wa kigeni, Sydney Shapiro.

Shtaka la nne, mshtakiwa anadaiwa kuiba dola 650 za kimarekani, simu moja ya mkononi aina ya IPhone 6, pamoja na dola 300 ambazo zilikuwa kwenye akaunti mali ya Lylia Garcia.

Yusuph anadaiwa, kuiba vitu hivyo baada ya walalamikaji hao kumkodisha kutoka Stesheni ya Tazara kwenda katika hoteli waliyokuwa wamekodiwa na mwenyeji wao na kwamba kabla na baada ya kujipatia vitu hivyo, alitumia nguvu ili aweze kujipatia vitu hivyo bila kizuizi.

Chanzo: Mwananchi
 
Hakimu Tarimo alisema ameridishwa na ushahidi wa mashahidi saba waliotoa mahakamani hapo dhidi ya mshtakiwa huyo.


Wanasheria naomba kufahamu, inapotokea washtaki ni raia wa kigeni kwa maana kwamba kesi inaweza kuwa imeahirishwa several time kwa ajili ya kukusanya ushahidi na yamkini wao wanakuwa wameondoka kurejea kwao, je kesi inaendeleaje wao wakiwa hawapo mahakamani
 
Kuna dhana mbaya sana kwa vijana wengi nchini kwamba wazungu ni dili. Hili limewafanya wengi kuhangaika ili wawapate na kuwaibia. Mwisho wa siku tunatangaza sifa mbaya nje ya nchi. Ukienda nje ya nchi unaipata hii sifa mbaya kwaTanzania. Kwahiyo hukumu hii kama ni ya haki basi ni sahihi maana itatoa fundisho kwa vijana wanaowaza na kupanga kunyanyasa watu kutokana na ugeni au rangi yao
 
Hivi hizi zilikuwag n stories tu kwamb mtu,kama amehukumiwa miaka 30 ni saw atakaa jela kwa miaka 15 kwamb wao masaa 24 ni siku mbili? Imekaej h mkuu?
Sina uhakika ila naona ni kama story tu kwani ya nini kusema miaka 30 wakati inageuka 15 wangetamka tu straight 15 ila nadhani kama tungesema parole hapo ndio zinapunguaga siku
 
Wanasheria naomba kufahamu, inapotokea washtaki ni raia wa kigeni kwa maana kwamba kesi inaweza kuwa imeahirishwa several time kwa ajili ya kukusanya ushahidi na yamkini wao wanakuwa wameondoka kurejea kwao, je kesi inaendeleaje wao wakiwa hawapo mahakamani
Mlalamikaji asipokuwepo kesi imekufa
 
Back
Top Bottom