Afungwa miaka 30 jela kwa kumpa mimba Dadake

Afungwa miaka 30 jela kwa kumpa mimba Dadake

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Charles Abel (24) Mkazi wa kijiji cha Usagara Mkoani Mwanza, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kwa makosa mawili ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la saba ambaye ni mtoto wa baba yake mkubwa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Misungwi, Erick Marley akisoma hukumu hiyo juzi alisema amechukua maamuzi hayo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Akitoa ushahidi mahakamani hapo, Mwanafunzi huyo aliiambia mahakama kwamba mnamo Juni 6 saa 1:30 usiku akiwa chumbani kwake aliingiliwa na kubakwa na kaka yake (Charles Abel) ambaye ni mtoto wa baba yake mkubwa.

Mshtakiwa akijijitetea mahakamani hapo, aliomba kupunguziwa adhabu akidai kuwa hawezi kufanya mapenzi na dada yake na kwamba ametengenezewa kesi hiyo.
 
Mambo ya mkoani hayaa
Ndizo kazi wanazoziweza hizo, kubaka vikongwe, dada zao mpaka wanawapa mimba, mauwaji ya albino na wazee wenye macho mekundu na ukatili mwingine wa kila aina! Wanaume wa mikoani wanaingoza.
 
Ndizo kazi wanazoziweza hizo, kubaka vikongwe, dada zao mpaka wanawapa mimba, mauwaji ya albino na wazee wenye macho mekundu na ukatili mwingine wa kila aina! Wanaume wa mikoani wanaingoza.
Wewe unautani wa jadi na watu wa mikoani
 
Dogo mjinga Sana, hyo ilikuwa ni ham Auujinga ,kwanini asinge jiunga na CHAPUTA, yeye anihisi sisi ni wajinga kujiunga na chama hicho?
 
Shangazi yenu anasemaje kuhusu hii sheria? Haijapitwa muda?
 
Dogo mjinga Sana, hyo ilikuwa ni ham Auujinga ,kwanini asinge jiunga na CHAPUTA, yeye anihisi sisi ni wajinga kujiunga na chama hicho?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] tumsamehe tu ila hajalewa sn huko aendako tutampelekea fomu
 
Back
Top Bottom