After Rape... Nini cha kufanya ?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

After Rape... Nini cha kufanya ?!

Discussion in 'JF Doctor' started by DAWA YA SIKIO, Dec 14, 2011.

 1. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Naandika uzi huu nikizingatia kuwa kuna matukio mengi ya ubakaji yanayotokea katika jamii yetu na mengi kati yake hayaripotiwi popote. Kuna sababu nyingi zinazopelekea hali hii kubwa ikiwa ni aibu,woga,kulindana na uelewa mdogo juu ya madhara yanayoweza kutokea kwa mtendwa kimwili na kiakili:

  ...YAFUATAYO YAKIZINGATIWA MTENDWA [SURVIVOR] ANAWEZA:

  • Kujiepusha na maambukizi ya Magonjwa ya zinaa na ya njia ya uzazi STIs/ RTI hata kama watenda/mtenda [attacker(s) ] walikuwa na maambukizo hayo.
  • Mtendwa anaweza kuepukana na maambukizi ya HIV hata kama ilikuwa apate maambukizo hayo katika tukio hilo.
  • Mtendwa anaweza akaepukika na mimba isiyotarajiwa hata kama ilikuwa awe mjamzito kufuatiwa na tukio lililomtokea.

  NINI CHA KUFANYA ?
  ... Ni muhimu kwa mtendwa kuwahishwa haraka kwenye kituo cha tiba. Huko yafuatayo yatazingatiwa:

  1. Uchunguzi utafanyika kubaini kama kuna ushahidi wowote wa sexual intercourse.

  2. Kama hakuna ushahidi wowote wa kitaalam unaothibitisha kuingiliwa kimwili,mtendwa anapaswa kufarijiwa na kuondolewa hofu.

  3. Endapo uchunguzi utaonyesha kuwa sexual intercourse ilifanyika
  mtendwa ataanzishiwa mara moja dawa ya kutibu STIs/ RTI. Tiba inaweza kuwa ya mseto ufuatao: inj penadur + tabs ciprofloxacin + tabs metronidazole + tabs azithromycin. Dawa hizo zinaweza kutolewa as a single high dose [ dozi kubwa ya mara moja].

  4. Kama tukio limeripotiwa ndani ya masaa 72 toka litokee mtendwa atashauriwa na kupimwa VVU.

  5. Kama majibu yatakuwa positive ataelekezwa sehemu husika ya huduma kwa wenye maambukizi [CTC].

  6. Kama majibu yatakuwa negative ataanzishiwa tiba iitwayo HIV PEP. HIV PEP imethibitishwa kutoa matokeo mazuri ya kukinga maambukizi dhidi ya VVU hata kama mtendwa atakuwa ametendwa na attacker(s) mwenye maambukizi,endapo tu masharti ya tiba yatazingatiwa,hii ni pamoja na kuanza matibabu ndani ya masaa 72. Kuendelea na tiba kwa muda usiopungua wiki 4. Kifupi katika HIV PEP mtendwa huanzishiwa aina flani za ARV ambazo atazitumia kwa mwezi 1. [ Nitaongelea zaidi HIV PEP wakati mwingine ikibidi].

  7. Endapo yatakuwa yamepita masaa 72 atapimwa kama kawaida. Kama ni positive atapelekwa CTC. Kama ni negative atafarijiwa na kuondolewa hofu.

  8. Kama tukio limetokea ndani ya masaa 120 na kuripotiwa kituo cha tiba kuna uwezekano mkubwa wa kuzuia mimba zisizotarajiwa ama utoaji mimba usio salama kutokea. Kinachofanyika mtendwa atapewa pills [vidonge vya uzazi wa mpango] katika high dose.
  eg.microgynon 4 tablets kutwa x2 kwa siku 1 AU Lo-feminal 4 tablets kutwa x2 kwa siku 1. AU Atawekewa kitanzi [copper IUCD] hadi pale atakapopata tena siku zake[menses].

  ... Kuna mambo mengi mengine ya kumfanyia kwa sababu for sure atakuwa pia amepata madhara mengine kimwili na kiakili,ikiwa pamoja na michubuko,maumivu ya kisaikolojia,woga,sonona[depression],dhamira ya kujiua ama kuua.

  ... Pia anatakiwa kufanyiwa uchunguzi tena baada ya miezi mitatu wa :
  > Via vya uzazi.
  > Vipimo vya HIV na Kaswende.

  AHSANTENI !!!
   
 2. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kuna dada mmoja alishauri unapokabiliwa na jaribio la kubakwa kuwa mpole na umpe jamaa kwa jam ili asikuumize. Abadai hii inaweza kupunguza hata uwezekano na michubuko na maambukizi! Sina uhakika ni rahisi kiasi gani kutulia na ukakata na kiuno....
   
 3. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  .... Hii inaleta ukweli flani. Kwa sababu ni rahisi zaidi kupata maambukizi endapo kuna michubuko. Ila cases nyingi za ubakaji huambatana na michubuko kwa sababu hufanyika bila ridhaa. Iko wazi tendo la ndoa ni la kisaikolojia zaidi. Sitegemei kama mtu anaebakwa na tension aliyonayo kama ataihimili hali hiyo na kuikubali kiakili. Sawasawa na kuambiwa ugonge msosi huku umesimamiwa na mtutu wa bunduki,tayari kuuwawa ukiishashiba. Sidhani kama utafurahia radha ya chakula hicho.
  Labda katika cases ambazo mtu amekuwa akibakwa kwa muda mrefu,so nae akachukulia kama
  sehemu ya maisha yake( so sad) !
   
 4. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Unapoelekea kubakwa: my take: kuwa mpole na jifanye unampa ushirikiano e.g: caressing. Katikahali asiyotarajia MMINYE MAP*MBU . Kumbuka kuyaminya hadi jamaa alegee kabisa! Looh Ujanja wote kwisha
   
 5. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi mbakaji huwa anakuja kwa ukali na hasira na huwa kama kichaa. Hapa mbakwaji awe mwangalifu, akijaribu kushindana naye anaweza kukabwaa kwa nguvu kwa nia ya kumzuia asimshinde na anaweza kumsababishia kifo au maumivu makali zaidi. Mbakwaji, anashauriwa baada ya kuona hana ujanja na jamaa ameshamdhibiti, ajilegeze tu ili apunguze uwezekano wa kuumizwa zaidi.
   
 6. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Lakini ukimminya yale maeneo unafikiri atakufanyaje tena kama siyo ku apologize?
   
Loading...