Afrika yangu na laana yake

kibokomchapaji

Senior Member
Aug 18, 2017
165
307
June 31, 2007.. Rais wa Zamani wa Libya Hayati Moummar Gaddafi akiwa amesindikizwa na Walinzi wake wa kike Waaminifu alihutubia ktk Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) jijini Accra- Ghana huku akiwa Amevalia Shati lake la Khaki lenye Picha za Wapiganaji na Waasisi wa Mataifa ya Afrika wenye Misimamo Mikali (Pan Africanists) kama Patrice Lumumba, Abdul Nasser,Julius Kambarage Nyerere, Kwame Nkurumah, Nelson Mandela,Sekou Toure, Thomas Sankara n.k,

Gaddafi akasema " Ndugu zangu Waafrika, tunapaswa kuchagua Moja aidha kuiunganisha Afrika yetu au kuruhusu ife, tunapaswa kuwa na Muunganiko wa Mataifa ya kiafrika na kuunda (United States of Africa), tuna kila kitu ndani ya Bala hili sasa ni vema tukaitimiza Ndoto hii, kwa kuwa Wamoja tunaweza kupambana na Ulimwengu wa Kileo"

Ndipo miaka kadhaa Baadae Gaddafi ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Afrika Mstaafu (AU),alivamiwa pale Libya...akauawa pale pale Libya kwa kile kilichopambwa na Mabeberu huku Ulaya na Amerika kwa neno "DIKTETA", neno ambao Mara zote Mabeberu na Vibaraka wamekuwa wakulitumia dhidi ya Viongozi wote wa Mataifa Machanga wanaojaribu kujinasua ktk Mtego wa Ukoloni wa Kiuchumi.

Kabla ya kuuawa kwa Ghaddafi Libya ilikuwa na Fedha Nyingi kuliko idadi ya Wananchi wake, Walikula na Kusaza na hata Fedha nyingine zikaelekezwa kuufadhili Umoja wa Afrika(AU),posho zote za Vikao na Mishahara ilitoka Libya, Fedha ya Libya ikafadhili Miradi mbali Mbali ya Maendeleo Afrika Nzima, Mabilioni ya Dollar yakatumika kumaliza Ghasia za Vita kule Niger na Mali, Baadhi ya Misaada tuliyopata Tanzania kama Nchi ni pamoja na kujengewa Msikiti pale Dodoma,

Leo Raia wa Libya wanasaga meno kwa Upumbavu wao, waliyakataa Maisha ya kifahari waliyoishi, Maisha ya kupewa Mishahara bila kufanya Kazi, kupewa Mke na kulipiwa Mahari na hata kupewa Nyumba uanze Maisha....Leo wana Laana na Damu ya Gaddafi na Chozi la Gaddafi juu ya Ardhi yao, ni Wapi kwenye Raha? Sirte? Tripoli au Benghazi?..Vurugu tupu.

Laana ya Gaddafi haijaliacha Bara la Afrika salama, imeanzia kwa Walibya na Sasa inagusa na Nchi zingine, Yaani Binadamu anauzwa dollar 400 haijalishi ni Profesa ama Memkwa, ana uwaraza,kiduku ama Zazuu...Walibya Wamechanganyikiwa!

Niseme Tu kwamba Biashara hii ya Utumwa wa Mtu mweusi ni ya kulaaniwa....na hata ingekuwa ya mtu mweupe ni laana pia, sasa tunauzana wenyewe kwa wenyewe...Sasa ni Wakati Sahihi AU Kuingilia kati....Kama Afrika na Viongozi wake walikaa kimya wakajifungia Majumbani Mwao bila kutoka Kauli wakati Mwenyekiti wake Mstaafu wa Afrika (Gaddafi) anavamiwa na kuuawa na Mataifa ya Magharibi,Je na hili la Mwafrika kumuuza Mwafrika Mwenzake kwa bei ya Tecno Phantom, tuvamie Libya au tuendee kubeba laana yetu?...inauma...GOD have Mercy Upon Us.

Pio Pius...2017.
 
Kweli kabisa. Waafrika ni kama tulilaaniwa hivi.
Mungu aingilie kati.
 
Waafrika sisi ni watu wa ajabu Sana,sisi tunakataa pema tunachagua pabaya.Watu wema tunawamaliza na kuwahifadhi wabaya.
 
Afrika ni kama George Floyd alivyowekewa mguu wa shingo. Hatuna maamuzi juu ya hatima yetu.
 
M
June 31, 2007.. Rais wa Zamani wa Libya Hayati Moummar Gaddafi akiwa amesindikizwa na Walinzi wake wa kike Waaminifu alihutubia ktk Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) jijini Accra- Ghana huku akiwa Amevalia Shati lake la Khaki lenye Picha za Wapiganaji na Waasisi wa Mataifa ya Afrika wenye Misimamo Mikali (Pan Africanists) kama Patrice Lumumba, Abdul Nasser,Julius Kambarage Nyerere, Kwame Nkurumah, Nelson Mandela,Sekou Toure, Thomas Sankara n.k,

Gaddafi akasema " Ndugu zangu Waafrika, tunapaswa kuchagua Moja aidha kuiunganisha Afrika yetu au kuruhusu ife, tunapaswa kuwa na Muunganiko wa Mataifa ya kiafrika na kuunda (United States of Africa), tuna kila kitu ndani ya Bala hili sasa ni vema tukaitimiza Ndoto hii, kwa kuwa Wamoja tunaweza kupambana na Ulimwengu wa Kileo"

Ndipo miaka kadhaa Baadae Gaddafi ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Afrika Mstaafu (AU),alivamiwa pale Libya...akauawa pale pale Libya kwa kile kilichopambwa na Mabeberu huku Ulaya na Amerika kwa neno "DIKTETA", neno ambao Mara zote Mabeberu na Vibaraka wamekuwa wakulitumia dhidi ya Viongozi wote wa Mataifa Machanga wanaojaribu kujinasua ktk Mtego wa Ukoloni wa Kiuchumi.

Kabla ya kuuawa kwa Ghaddafi Libya ilikuwa na Fedha Nyingi kuliko idadi ya Wananchi wake, Walikula na Kusaza na hata Fedha nyingine zikaelekezwa kuufadhili Umoja wa Afrika(AU),posho zote za Vikao na Mishahara ilitoka Libya, Fedha ya Libya ikafadhili Miradi mbali Mbali ya Maendeleo Afrika Nzima, Mabilioni ya Dollar yakatumika kumaliza Ghasia za Vita kule Niger na Mali, Baadhi ya Misaada tuliyopata Tanzania kama Nchi ni pamoja na kujengewa Msikiti pale Dodoma,

Leo Raia wa Libya wanasaga meno kwa Upumbavu wao, waliyakataa Maisha ya kifahari waliyoishi, Maisha ya kupewa Mishahara bila kufanya Kazi, kupewa Mke na kulipiwa Mahari na hata kupewa Nyumba uanze Maisha....Leo wana Laana na Damu ya Gaddafi na Chozi la Gaddafi juu ya Ardhi yao, ni Wapi kwenye Raha? Sirte? Tripoli au Benghazi?..Vurugu tupu.

Laana ya Gaddafi haijaliacha Bara la Afrika salama, imeanzia kwa Walibya na Sasa inagusa na Nchi zingine, Yaani Binadamu anauzwa dollar 400 haijalishi ni Profesa ama Memkwa, ana uwaraza,kiduku ama Zazuu...Walibya Wamechanganyikiwa!

Niseme Tu kwamba Biashara hii ya Utumwa wa Mtu mweusi ni ya kulaaniwa....na hata ingekuwa ya mtu mweupe ni laana pia, sasa tunauzana wenyewe kwa wenyewe...Sasa ni Wakati Sahihi AU Kuingilia kati....Kama Afrika na Viongozi wake walikaa kimya wakajifungia Majumbani Mwao bila kutoka Kauli wakati Mwenyekiti wake Mstaafu wa Afrika (Gaddafi) anavamiwa na kuuawa na Mataifa ya Magharibi,Je na hili la Mwafrika kumuuza Mwafrika Mwenzake kwa bei ya Tecno Phantom, tuvamie Libya au tuendee kubeba laana yetu?...inauma...GOD have Mercy Upon Us.

Pio Pius...2017
Magufuli bado hajawa mtu wa kufananisha na Ghaddafi. Ameharibu nchi hii vibaya.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom