Afrika ya leo, siyo kama ya jana

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,209
4,406
1)Afrika yetu ya leo,siyo kama ya jana.
Binadamu wauwana
Kikatili wachinjana.hakuna hurumiana .
Wote wanakalaumyana.
Afrika yetu ya kesho,haitokua ya leo.

2)Afrika yetu ya leo,siyo kama ya jana.
Ukatili kila kona.
Waasi wamejazana.
Magaidi wanatuna.
Pakujificha hakuna.
Afrika yetu ya kesho,haitokuwa ya leo.


3)Afrika yetu ya leo,siyo kama ya jana.
Demokrasia laana.
Yafanya twaumizana.
Madaraka twa pigana.
Na ngozi tunachunana.
Afrika yetu ya kesho,haitokuwa ya ya leo,siyo kama ya jana.
Wakoloni wa mabwana.
Kimya kimya watukana.
Bara halina maana.
Etu fikita hatuna.
Afrika yetu ya kesho haitokua ya leo.



5)Afrika yetu ya leo,siyo kama ya jana.
Poleni waso ungana.
Wanaopenda tengana.
Wota ndoto za mchana.
Afrika yetu ya kesho,haitokua ya leo.




Shairi=Afrika ya leo.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom