Afrika na siasa zake

Afrika na siasa zake

Apollo one spaceship

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2021
Posts
246
Reaction score
457
Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali za jamii, kama vile mji, taifa, au hata dunia nzima (siasa ya kimataifa).

Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.

Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi.

Siasa za kitaifa Afrika Mara nyingi,hatima yake huamuliwa na jamii ya kimataifa hasa nchi za Magharibi ambao kama wafadhili wetu wanaweza kupinga au kuyapitisha maamuzi yetu kulingana na jinsi watakavyonufaika wao(Mabeberu).

Tafasiri ya hapa Ni kwamba Mabeberu watatunyonya kwa asilimia mfano 98 kwa kila asilimia 2 ya maendeleo tunayopiga.

Kwa hiyo,tutapoteza muda kwenye majukwaa,kwenye matamasha,kubishana kwenye social media,kwenye mikutano,kwenye semina lakini mwishowe MABEBERU watafinyanga maamuzi au sera tulizoweka ili wanufaike wao.

Hapa lazima tukubaliane na matakwa yao kama tutahitaji kufadhiliwa.Kibaya zaidi ufadhili wenyewe una masharti kama riba kubwa kwenye mikopo yao nk.

Hapa Ni sawa na mwajiri na mwajiriwa,ambapo mwajiri huwa anafanya kila namna ili mwajiriwa adumu kumtumikia hata kama maisha yake yote.

Hivyo,mwajiri atampa mshahara mdogo,atamunyima elimu ya kujikomboa kifikra nk.

Kwa hiyo tunaweza bila shaka yoyote kusema tu kwamba sisi Ni waajiriwa ambapo maboss wetu Ni mataifa ya Magharibi.

Kwa maelezo hayo nadiriki kusema kwamba siasa kandamizi kama hizo ambapo mataifa ya Magharibi ndio hupuliza kipenga cha mwisho zilifahamiwa kwa undani na hayati JPM,hayati Muammar Ghadaffi,hayati Sankara na wengine wengi ambao walifyekelewa mbali na Mabeberu.

Hayati JPM alizifahamu siasasiasa hizi, na kwa uzoefu wake kwenye utumishi bila shaka aliziheshimu sana,Lakini kwa kuzingatia kwamba matokeo ya siasa hizi mwishowe Ni kupitishwa kwenye chujio la kibeberu: Yeye hakupata tabu alidiriki kutekeleza kile alichoona kinahitajika kwenye taifa lake kama hii MIRADI MIKUBWA ambayo ingeonekana batili kwenye macho ya kibeberu,endapo ingejadiliwa kisiasasiasa sana.

Matokeo ya maamuzi haya ya hayati JPM kwa wanasiasa vipofu na yumkini vibaraka wa Magharibi(au wengine kufanya siasa za mkumbo) ni kwamba walitafasiri kama uvunjifu wa sheria,kubana uhuru wa habari,kukiuka itifaki nk.

Kwa mtazamo wangu(sio wako) hiki walichotetea kilikuwa sahihi lakini cheza wacheze mwisho wa siku sisi kama taifa tungekutana na mizani (baada ya vioja na vijisiasa vyetu) ya MABEBERU ambayo imekuwa kikwazo cha maendeleo yetu kwa miaka mingi.

MWISHO Nadiriki kusema kwamba;
##Sambamba na ujenzi wa taasisi bora za ndani zenye kuwajibika,zisizo na rushwa nk(ambapo ktk hili hayati JPM alijitahidi kwa kiasi chake),tusipoangalia namna ya kukomesha unyonyaji wa kibeberu bila kuathiri mahusiano yaliyopo,tutegemee kulamba viatu vya ndugu zetu wamagharibi kwa miaka mingi.

##African politics and most democratic views are there for self destruction of the continent.Kumbukeni hivi vijisiasasiasa tumeletewa na wamagharibi wenyewe kwa hiyo tumekuwa wa kufata mkumbo tu.

##Tuache maisha ya kuigiza.Tuishi maisha yetu halisi kiuchumi na kijamii.Kama unaona Jambo Lina tija kitaifa punguza propaganda.Baadhi ya wanasiasa wetu wanapenda misifa!!(kwa kuonekana wanajua kujenga hoja kuliko dunia nzima).Kuna watu wana hoja nzuri lakini wanawazoom tu

##Tukitaka maendeleo ya kweli Kuna vitu lazima tuvisacrifice(nadhani tunaelewana).Hata kwenye maendeleo yake kama mtu binafsi MO dewji Kuna vitu alisacrifice ili awe tajiri mfn starehe(mfano tu);sembuse sisi kama taifa

##Sijazikataa siasa zetu ila tukumbuke kuwa Mabeberu ndo waamuzi wa mwisho

##Njia kuu ya kumkomboa mwafrika Ni yeye kuwa na uchumi wake wa kujitegemea kwa kufanya utafiti kwenye sayansi na teknolojia.Wasomi watafiti miti ya madawa ,watafiti madini,wabuni mashine nk.Tuwekeze kwenye elimu ya darasani kwa miaka michache Kisha tuingie kwenye vitendo.Swala la kukaririshana material ya darasani kwa miaka mingi Ni utumwa wa kifkira.

##mimi si mkamilifu,hivyo kama mawazo yangu yanakukwaza,naomba uendelee kuwaza wewe kama wewe##Sijapandikizwa chuki dhidi ya MABEBERU ila uonevu wao kila mwenye jicho anauona au kuusikia
 
Siyo siasa za Afrika ni sihasa za chato,msoga na makunduchi.
 
Back
Top Bottom