Afrika Kusini yaongoza ujangili wa Faru

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,481
1,364
Mahitaji ya pembe za faru yamesababisha kuongezeka kwa ujangili mwaka huu nchini Afrika Kusini, shirika la wanyama pori WWF limesema.
Takwimu kutoka Mamlaka ya Hifadhi za Wanyama Afrika Kusini zinaonyesha kuwa faru 341 wameuawa hadi kufikia 2011, ikipita idadi ya mwaka jana ya 333.
[h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]



WWF linasema kiwango kikubwa cha ujangili Afrika na Kusini mwa Asia kinasababishwa na mahitaji ya pembe za faru kwa dawa za kinyeji nchini Vietnam.
Majangili wanachomoa pembe ya faru huku wakimwacha mnyama huyo anavuja damu mpaka kufa.
Katika miaka mitano mpaka 2005, kiasi cha faru 36 waliuawa kila mwaka Afrika Kusini.
Shirika la WWF linasema usimamizi wa sheria unaongezeka lakini hakujawa na hatua madhubuti za kupambana na magendo na uuzaji wa pembe hizo unaofanywa na uhalifu wa magenge.
Afrika Kusini imekuwa kitovu cha ujangili kwa sababu ya idadi kubwa ya faru duniani, ikiwa na faru 1,916 weusi na 18,780 weupe, shirika la hifadhi la Wanyama limesema.
Biashara ya pembe za faru inaratibiwa na Shirika la Hifadhi ya Wanyama na Biashara ya Kimataifa ya Wanyama walio hatarini (Convention on International Trade in Endangered Species -Cites) na kwa sasa Afrika Kusini pekee ndio yenye kibali cha kuruhusu uuzwaji wa pembe za faru nje ya nchi.
WWF kinasema kuna haja ya kuimarisha uratibu wa vibali vya kuwinda na usimamizi wa ghala za pembe za faru nchini humo.
"Kwa kuwa ulinzi wa silaha unaosimamia Faru katika Hifadhi za wanyama nchini Afrika Kusini ni mkalu, mitandao ya majangili ina uwezekano wa kuhamishia shughuli zao nchi nyingine ambazo hazisimamii sheria zake zikiwemo nchi za Asia," Carlos Drews, Mkurugenzi wa Viumbe duniani wa WWF, ameonya katika taarifa yake.
Serikali ya Afrika Kusini imekasimu utafiti ufanyike kujua kama kuhalalisha biashara ya pembe za faru inaweza kusaidia kupunguza ujangili.
Nchini Vietnam wengi wanaamini kuwa pembe za faru zinaweza kutumika kutibu saratani ingawa hakuna uthibitisho wa kisayansii na pembe zinazoplekwa Mashariki ya Kati zinatumika kutengenezea vishikio vya majambia yenye mapambo.

source bbc
 
Back
Top Bottom