Afrika imerogwa na nani?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,619
  • Ian Khama - Ufisadi, silaha na utakatishaji fedha.
  • Cyril Ramaphosa - Utakatishaji fedha, uhujumu uchumi na ujangili, akihusishwa na Arthur Fraser.
  • Jacob Zuma - Matumizi mabaya ya ofisi na rasilimali, ameponzwa na state capture ya Ajay Gupta.
  • Paul Biya - Umri miaka 90 ameng'ang'ania ikulu.
  • Isabel Dos Santos - Tajiri mwanamke Afrika.
Afrika ni tamu sana kwa wenye madaraka na ukwasi lakini ni shubiri kwa hustlers. Vipi tu-import viongozi toka Ughaibuni?

Afrika imerogwa na nani?
 
Hao watawala ndio tatizo wanaamini madaraka na mali ya umma ni haki yao kula.
 
Pia kuna Mu7, PK, CCM, Salva Kiir! Ni shida tupu.
 
Sio kurogwa ! Tatizo ni Akili finyu inawapelekea kuwa Selfish !! Binti ya Do Santos bilionea wa kwanza mwanamke Africa ana kesi ya kujichotea madolari kibao kipindi cha Baba yake akiwa madarakani. !! Tamaa mbaya bandugu na maisha ni mafupi tu hata ukichota ngapi !!
 
Hao watawala ndio tatizo wanaamini madaraka na mali ya umma ni haki yao kula.
Africa haijawahi pata uhuru, bali wakoloni walibadilisha jinsi ya kuitawala Africa...Wakaweka vibaraka kwa akili sana ili waendelee kututawala kupitia hao....Its so saaad!

Mpka Africa ipate uhuru wa kweli, ndipo tutapata mifumo thabiti ya kutuongoza...Vizazi vya leo visipong'amua haya vitaendeleza statusquo
 
Humu humu unaona mtu hata mbele wala nyuma hana, ndugu zake wote masikini lakini yupo busy kulamba viatu vya wenzake ili ale masazo i.e makombo ya walio high table...What a cheap mentality!
 
Huu mfumo ni wa Dunia nzima...

Hakuna nchi iliyo salama na haya mambo... hakuna binadamu mkamilifu

Tumeona mengi sana kuanzia huko kwa nchi za asia, nchi za ulaya na marekani

Mifano ni mingi sana... Juzi sakata linalo endelea ni kumuondoa mwana mama wa umoja wa ulaya kwa kula rushwa kutoka uarabuni huko

Wakina Platin na Blatter wameondolewa kwa kashfa kama hizo

Wakina messi, neymer nk wamekutwa na makosa yanayo fanana na hayo

PSG imevunja sheria mbalimbali za financial lakini kwa nguvu ya pesa imeweza kukwepa lungu...

Korea na japan wamekutwa na mambo kama haya sana, huko amerika ya kusini ndio balaa...

Urusi tume jionea kwa vipindi tofauti vya kiutawala kwa kurejeshana madarakani kishikaji ili kuendelea kula nchi...

Na nchi zingine za western europe...

Rais na councellor schortz wa ujerumani wana chunguzwa kwa viashiria kama hivi, hasa bwana schortz kipindi alikuwa kiongozi pale hamburg...

Familia za kifalme kuanzia uingereza, spain, uholanzi nk zina pigwa vita na wananchi wao sababu ni hizi za kujilimbikizia mali na madaraka...

Huko marekani kuanzia CIA mpaka ikulu ni majanga matupu... mabosi kadhaa wa CIA walisha wahi kukutwa na tuhuma kama hizo, na marais kadhaa walitumia vyeo vyao vibaya kama huyu ndugu Trump kukwepa kodi nk...

Haya mambo ni dunia nzima... sema wengine wana shindwa kucheza karata zao vyema ndio maana wanakutwa na majanga kama wakina

Al bashir kakutwa na mapesa ndani
Wakina gadaf
Huko misri tunisia na kwa mfalme wa morocco ni yaleyale kama ya nchi zingine na urusi juzi walivyo kuta pesa za tani kadhaa kwenye shangazi kaja...

Waafrika tuna jizalau sana... dunia ni hii hii haina yofauti, yofauti ni jinsi ya kujilemba lakini ndani huko takataka ni zilezile, mavi, mikojo, kamasi, mate nk
 
Ongeza na hii:-
Magufuli CAG query Tsh 2.4 Trillion
 
Huko kote ulikotaja hawana umasikini wa kuulinganisha na Uliopo bara la Africa !! Kama matajiri wanaibiana wao kwa wao haina shida sana lakini wanapoibiwa masikini hapo ndipo shida inakuwa kubwa sana !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…