Afrika haiwezi kufanikiwa kiviwanda

Afrika haiwezi kufanikiwa kiviwanda

The seer

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
407
Reaction score
690
Kwa sasa ni bara LA afrika pekee ambalo halijafanikiwa kiviwanda,siku za nyuma Asia pia ilikuwa nyuma kiviwanda lakini kwa sasa wamepiga hatua kubwa sana kiviwanda mfano wa nchi za japan, china south Korea,Singapore,India .n,k.
Hivyo basi changamoto kubwa waliyonayo mabara yaliendelea kiviwanda ni soko( market) kwa ajili ya bidhaa zao.kinachofanyika sasa kwa mabara hayo ni kugombania soko LA afrika,scramble for african market) bara LA afrika asilimia zaidi ya 90 ya bidhaaa huagiza nje.hivyo mataifa yote yanaligombea bara LA afrika ili wauze bidhaaa zao.
Mabara makubwa ya ulaya America na Asia wanatumia kila mbinu kuua viwanda vya afrika ili wauze bidhaaa zao.hawatokubali kamwe tuwe na viwanda.wao hupenda tuwe na viwanda vidogo vidogo vya juice za ukwaju.peremende,n.k
Pia kuwaua viongozi wenye maono yakuikomboa afrika kama gadafi.kwame nkuruma .n.k
Pia kutoa misaada na kutupangia nini cha kufanya.
Kwa sasa nchi ya china imefanikiwa kuteka soko LA afrika kwa kuleta bidhaa feki kwa bei ndogo sana.
Malengo yao afrika ibaki sehemu ya kuchukua malighafi mbalimbali kwa ajili ya viwanda vyao.
ukiona biashara au kiwanda kikubwa kimefanikiwa afrika basi mizizi yake iko ulaya au Asia au America,mfano cocacola na pespsi mizizi iko marekani,dstv mizizi iko britain, ni viwanda vichache vikubwa vya asili ya afrika ndio vimefanikiwa kama dangote group.
Siku chache mfanyabiashara mkubwa afrika aliko dangote alikiri kuwa china inaua viwanda vya afrika maksudi kwa kuleta bidhaa feki kwa bei ndogo.
Kwa Tanzania tuendelee kumuombea rais wetu ili afanikiwe katika maono yake ya kuwa nchi ya viwanda.kwani ni maono mazuri.

Afrika inapaswa iamke toka usingizi wa miaka 2000.
Kwa
1.kusomesha wataalam wengi ili tuwe na wavumbuzi na great thinker na think tank.
2.Kupokea zaidi misaada ya kiujuzi na kitechnologia kuliko misaada ya kipesa inaisha kupitia rushwa na kuishia kwenye mchakato na upembuzi yakinifu.
3.kuwezeza zaidi kwenye elimu bora.
4.kuungana afrika na kuwa na pesa yetu African dollars
5.Kuucha migogoro na tamaa ya madaraka inayopelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe.
6.kutokomeza magonjwa,magonjwa yanaathili sana nguvu kazi,afrika magonjwa ni mengi sana hata wewe msomaji unaumwa sema kwenda hospitali mpaka uzidiwe saba unamezi panado tu.ulaya watu huenda hospitali Mara 2 kwa Mwaka hata kama haumwi chochote kucheki afya,wajapana huenda Mara 4 kwa Mwaka ili kucheki afya tu.ukiona mwafrika ameenda hospitali ujue anaumwa sana.
 
viwanda vya nn kwanza vinaleta madhara>>>>>mabadiliko ya Hali ya hewa pamoja na magonjwa kibao kwa bidhaa za vyakula vilivyosindikwa makansa yenye ujazo ona China wanavyohaha kutafuta hewa safii
 
viwanda vya nn kwanza vinaleta madhara>>>>>mabadiliko ya Hali ya hewa pamoja na magonjwa kibao kwa bidhaa za vyakula vilivyosindikwa makansa yenye ujazo ona China wanavyohaha kutafuta hewa safii
Ila Kumbuka nchi zilifanikiwa ni kwa sababu ya viwanda,case study china
 
maendeleo ya viwanda yana mapinduzi ya muda mrefu sana sio fumba fumbua viwanda hivi hapa! sera ya awamu ya nne ilikuwa inauwezo wa kutuvusha kimaendeleo zaidi.
ukisikia hadi mtu anasema "ukiwa na cherehani mbili ni kiwanda" elewa hali ishakuwa tete hapo
 
Back
Top Bottom