Afrika haitaendelea kamwe?

Afrika haitaendelea kamwe?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,652
Reaction score
5,134
' tusipoziba ufa tutajenga ukuta'

binadamu aliumbwa pekee kwa udongo uliofinyangwa na baadae ubavuni mwake alitolewa mwenza kwa ajili ya kuijaza dunia,nimenukuu maneno machache kutoka vitabu vya dini lengo ni kuonyesha asili ya neno binadamu na sifa zake kuwa ni kiumbe dhaifu na humtegemea mwengine ili kujifanikishia mipango yake.

Ukoloni

Ni kipindi ambacho afrika ilishuhudia uvamizi wa kimabavu na kutawaliwa katika kipindi hichi ilitengenezwa misingi ya kudhoofisha akili na nguvu kazi kwa lengo la kuendeleza dhima ya kutawala katika mfumo mzima wa maisha.haikutosha kwa muda wa miaka kuzitawala nchi nyingi za afrika ila misingi iliyoanzishwa iliendeleza utumwa na ukoloni hadi kufikia sasa.

Siasa

mfumo mzima wa uongozi na utawala katika nchi nyingi za afrika hazijaweza kuwa rafiki kwa mazingira tendaji wa nchi hizi,bali mfumo uliopo ni wa kuunda vibaraka ndani ya nchi kwa maana hiyo ni vigumu sana kwa mfumo wa kisiasa ambapo tumeupokea kuendana na mazingira yetu.afrika ni masikini na silaha ya tajiri ni kipato na hawezi kuendelea kumaintain status kama haendelea kukudumaza.wazungu ni maadui wakubwa kwa maendeleo tumeshatoa haki zetu kwa kuwapa nguvu kubwa ya kiutendaji katika nchi zetu.

Uchumi

misingi ya uchumi wa kidunia haijawahi kuwa salama na rafiki kwa hizi nchi masikini na kadri tunavyozidi kujisogeza ndiyo wanazidi kuharibu uchumi kwa njia zao za propaganda kuua masoko ya uzalishaji kwa muda ili kulitingisha dunia.

mapendekezo yangu hakujawahi kuwa na urafiki wa hali kinzani au matabaka ila upo uhusiano wa kimaslahi kwa matabaka haya ila muathirika ni tabaka la chini,ndivyo hivyo nchi za afrika hazitofaniukiwa kujikomboa katika vita ya kiuchumi,kijamii,siasa n.k kama tukijenga uhusiano zaidi na wazungu ila linachotakiwa ni kuongeza nguvu kazi na ubunifu katika kila changamoto mfano siasa tunahitajika kurudi kwenye mfumo wetu wa baada ya ukoloni ambapo tulifanya reforms nyingi ambazo zingetruwezesha kujiendesha lakini zaidi uchumi.
 
Maendeleo ya naanza na wewe mwenyewe badaye nchi yako Tz, then ndo ongelea Africa, achana bara la Africa ni pana na ni complicated sana, focus Tz kwanza
 
Back
Top Bottom