African woman looking white! What went wrong with us?

Zuluu "blackmail,black spirit don't forgot devel is black too,black money"
 
Mkuu weupe au weusi hizi ni rangi tu na ndio maana kuna watu wanasifiwa au kujisifia kwa aina ya weusi wao na wengine weupe wao,napinga hoja ya kwamba et wanataka kuwa kama wazungu. Mtu akijichubua mnasema anataka kuwa kama mzungu kana kwamba hakuna waafrika wanaozaliwa wakiwa weupe kabisa,weupe ni rangi tu kama mtu amejibua ili awe mweupe kwanini tuone anajidharau na kutaka kuwa mzungu?
 
Kuna watu mahali fulani huko wakitaka kuoa huwa wanatafuta "A blonde woman" sasa labda huyo mdada kapata mtu wa pande za huko.
 
Sasa kwanini utumie madawa kujikoboa uwe mweupe kama zote ni rangi?? Mbona wazungu wako happy na mangozi yao ya kiti moto?? Tukubali sisi waafrica tuko weak na tunaona kama tulivyo ni laana.
Sasa hivi wadada wa mjini hata nywele, kucha, kope kila kitu fake.
 
Nimeshakwambia hata huku afrika kuna watu wanazaliwa na rangi nyeupe kabisa ila wewe umekazania weupe na uzungu tu ni wazi wewe ndio unaejiona unalaana ukijilinganisha na mzungu na ndiyo maana kwako wewe weupe ni uzungu na kila kitu jambo unawataja wazungu tu. Hao wazungu nao wanaweka kucha feki,kope fake,wanavaa mawigi na hadi wana shape fake. Hayo yote ni urembo tu ila akifanya muafrika hayo unaona anataka awe mzungu na si kwamba anafanya kama urembo tu.

Unaweza kukuta mwanamke kajichubua ila anamsifia mwanamke mwenzake mwenye rangi nyeusi kuwa ana weusi mzuri,sasa wangekuwa wanajibua kwa sababu hizo unazozieleza basi wasingesifia ngozi nyeusi tena,weusi au weupe ni rangi tu na ndiyo maana kukuta mzungu mbaya pamoja na weupe wake hivyo watu hawajichubui ili wawe kama wazungu wala waarabu bali wanataka wawe na ngozi nyeupe hata warangi au wachaga wanazo.
 
Something went wrong with Africans! Mtu anajiunda anakuwa na rangi kama mzimu.
Unachofanya ni ubaguzi wa rangi sasa,kuna mzungu amebadili ngozi na kuwa mweusi sasa sipati picha watu weupe huko waseme huyo mwanamke amebadili ngozi kawa kama nyani,nadhani hapo utaona waafrika wanavyotokwa mapovu.
 
Kuna Waafrika Weupe na Weusi
Kuna Waarabu Weupe na Weusi
Kuna Wahindi Weupe na Weusi
Sijawahi kumwona Mwarabu au Mhindi Mweusi akiichukia ngozi yake nyeusi na akafanya juhudi ya kubadilisha ngozi yake iwe ya rangi nyeupe.
Wote wanazipenda na kuzithamini rangi zao za asili.
Tatizo lipo kwa Mwafrika Mweusi, kuna baadhi ya Waafrika weusi hawauthamini weusi wao.
Wanalazimika kuharibu ngozi zao ili ziwe Nyeupe.
Hii ndio tofauti ya Waafrika.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lupita nyong'o mtoto wa prof. Anyang' nyong' wa Kenya pamoja umaarufu wake duniani kwenye tasnia ya uigizajiii adi kutwa tuzo ya Oscar bado anajivunia rangi ya asiliii, sijui nini kimewasibu awa Dada zetu apa kwetu bongo
 
Sio kwamba wasiojichubua basi wanapenda na kuthamini ngozi zao,mwengine anaweza asiipende ngozi yake nyeusi ila asiamue kujichubua.
Hivyo kujichubua ni uamuzi wa mtu tu,unakuta mtu hajichibui na anawaponda wanaofanya hivyo ila yeye huyo huyo anaogopa kutembea kwenye jua kali kisa atakuwa mweusi sana,sasa mtu kama huyo utasema anathamini ngozi nyeusi?
 
Tatizo tuliaminishwa vyeupe ndio salama/vizuri


VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
 
Lupita nyong'o mtoto wa prof. Anyang' nyong' wa Kenya pamoja umaarufu wake duniani kwenye tasnia ya uigizajiii adi kutwa tuzo ya Oscar bado anajivunia rangi ya asiliii, sijui nini kimewasibu awa Dada zetu apa kwetu bongo
Kujichubua ni uamuzi wa mtu tu,sasa kisa Lupita hajajichubua ndio useme anajivunia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…