Katika historia ya Dunia hakuna mtawala aliyewahi kufanya maamuzi yakawa sawa 100% au yakawapendezesha wote. Labda kama mnamfahamu mniambie Nkurumah vile vile alikuwa na matatizo yake...Soma Historia zaidi na utaafiki kwa maelezo hayo basi tukubali Nyerer hakuwa kamili pia ila kuna watu ambao walitaka nyerere sikosea hata kitu kimoja..sasa hiyo haiwezakani lakini katika ulinganisho wa mwisho mazuri ya nyerere yanazidi mabaya aliyotenda na ni viongozi wachache sana wa kiafrika wakati huo unaweza kuwaweka katika mizani sawa na nyerere. He was extraordinary on the other was he was not ordinary.
Kuhusu Umoja wa Afrika Nyerere pekee hawezi kulaumiwa na hapa ninamaanisha hata angekuwa upanda wa nkrumah haimaanishi umaja wa afrika ungeafikiwa. Je labda uniambie kama walipiga kura ratio ya proposing na opposing ulikuwa ngapi? sasa kwa nini kelele hizi? Nyerere ,..nyerere kila siku .Huyo Nyerere hakuwa Mungu na hata angeunga mkono kula yake ilikuwa ni moja tu na haimaanishi vilevile huo muswada ulishidwa kwa kula moja.
Nyerere asilaumiwe labda mlaumu kizazi chote cha utawala kipindi hicho. Halafu Winston Churchil alisema ' Ukianzisha ufitini kati ya wakati huu(present) na uliopita (past)uko kwenye hatari ya kushindwa wakati ujao(future). Ndugu tuangalie mbele, Tuangalie Je Gaddaffi ataweza? Kikwete atasaidiaje? na marais wengine watasaidiaje na Je itawezekana? au ni day dreaming?