From AZAM page
Tumejikoki kwa kuingiza software mpya kwenye decoder yako itakayokuwezesha kufaidi uhondo mpya na burudani nyingine kemkem zitakazoanza rasmi hiyo Machi Mosi.
Punde baada ya kuingiza software hiyo mpya, sasa mdau wetu umepata ongezeko la channel mpya za TV zifuatazo:
1. Liverpool TV ( Service no : 403 )
2. Real Madrid ( Service no : 403 )
3. MBC Power Plus ( Service no : 403 )
Lakini hizi zitafunguka rasmi ifikapo tarehe 1 Machi 2015
Redio:
1. EFM (Service no : 51)
2. TIMES FM (Service no : 52)
3. TBC FM (Service no : 53)
4. CHOICE FM (Service no : 54)
5. ABM FM (Service no : 55)
6. RADIO UHURU (Service no : 56)
Licha ya ongezeko hili, sasa mdau wa azamtv utapata channel nyingine ambazo si za kifurushi chetu cha azamtv bali ni channel za bure ambazo zinarusha matangazo yake kupitia satellite ile ile itumiwayo na azamtv ambapo software yetu mpya itakuwezesha kuzipata bureeeeeee!!!
Channel hizo za bure ni hizi zifuatazo:
Africa TV 2
Peace TV English
Quran TV
Sunna TV
IBN TV
TV Imaan
Movie Africa Unite
Revelation TV
Muvi Prism Africa
Muvi Nkhani
Movi Yanga(Hope Channel Zambia)
Movi Emmanuel (Emmanuel TV)
(Hizi zitakuwa kwenye list ya Other TV Channels)
Kile kilio chenu cha channel za dini...sasa kimekwisha!!
(Hizi zitakuwa kwenye list ya Other TV Channels)
Redio:
Hot FM Radio
Radio Maarifa
Komboni Radio
Kuna uwanda mpana sana sasa, kwanini tusiwatafutie ile kitu roho inapenda???
Pamoja na hayo, software hii mpya itaboresha yafuatayo:
Kuweka logo nyepesi ya AzamTV (watermark logo) kwenye video na maboresho mengineyo madogo madogo.
Ku update channel au software bila kukuletea ujumbe wa kukutaka uapdate (Tuta update wenyewe moja kwa moja) wewe endelea kuburudika tu!!
Sasa ili kuingiza software hii mpya fanya yafatayo:
Zima decoder yako kutoka kwenye umeme (Yaani kwenye switch) subiri kwa dakika kisha washa, Basi hapo utakuwa umemaliza!!!
Punde decoder yako ya azamtv ikiwaka, utapata huo uhondo mpya woooteee!!! Ni rahisi kabisa!!
Au kama umeletewa ujumbe wa kukubali ku update software hiyo mpya kubali kwa kubonyeza Yes, kisha baada ya hapo hutopata ujumbe huo tena!!!Kila update au channel itaingia moja kwa moja (Automatic) bila usumbufu wowote!!
Kingamuzi kikimaliza kufanya update, bonyeza OK na uende kwenye Other TV Channels kwa kubonyeza mshale wa kuongezea au kupunguzia sauti utaona ongezeko hilo la channel mpya za bure.
Acha burudani iendelee....
Tumejikokiii!!!.
Meanwhile in kenya noone is mising the three muskerteers, guys have moved on and have discovered they can do without them