Africa tunahitaji "MANAGERS" badala ya LEADERS".

Africa tunahitaji "MANAGERS" badala ya LEADERS".

FYATU

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
5,867
Reaction score
5,064
Waafrika ni jamii tuliyokwisha ithibitishia Dunia na hata kujithibitishia wenyewe kuwa kuna tija ndogo sana kutoka Viongozi wao.

Chaguzi zimekuwa vichaka tu, ndio maana leo utashangaa nchi iliyotawaliwa na Kiongozi mmoja miaka 40 siku anapinduliwa ndio utawasikia wananchi wanashukuru kwamba walishachoka,na chaguzi zilikuwepo na huyo Raisi alikuwa anashinda tu kwa kishindo.

Na si kwamba eti anayeingia ataleta unafuu,la hasha mambo yanaweza kuwa yaleyale au hata kuharibika zaidi.

Uongozi umekuwa mali ya kundi fulani tu, ikitokea wanahitilafiana na Wenzao basi nchi itatumbukia kwenye vikundi vya uasi.

Ni bora Afrika kuajiri Mameneja kwa taaluma zao bila kujali wanatokea nchi au bara gani,wasimamie rasilimali na raia wagawane kwa haki.
 
Kuna wadau humu JF hudai tulitakiwa tuwe colonized mpaka sasa pengine tungalikuwa mbele kidogo....

Kwa mantiki hiyo ndio uzi wako unaelezea hivyo

Anyway naungana na wewe moja kwa moja kutoka L.A
 
Tuna miaka zaidi 60 lakini tumedumaa kimaendeleo kwa watawala wamekosa vision wamebaki na ubabe wa kulazimisha mambo
 
Kuna wadau humu JF hudai tulitakiwa tuwe colonized mpaka sasa pengine tungalikuwa mbele kidogo....

Kwa mantiki hiyo ndio uzi wako unaelezea hivyo

Anyway naungana na wewe moja kwa moja kutoka L.A
Kuwa colonized ni kuwa fully chini ya Mamlaka ya nchi nyingine.

Hicho sicho ninachojaribu kumaanisha hapo. Mimi ningetamani Africa iendeshwe kama Kampuni ambapo Manager atasimamia
mambo yote mpaka ya kiutawala kama Muajiriwa, akimaliza muda wake anakuja mwingine.

Kampuni itakuwa na idara zake,nazo zitasimamiwa na Mameneja wenye taaluma husika,mfano Idara ya Nishati atakaa Mtaalamu wa Nishati n.k.

Rasilimali zote za nchi zitasimamiwa na kila baada ya muda tuliokubaliana Wananchi tutasomewa mapato na Matumizi.

Meneja na Wasaidizi wake wataishia kwenye mishahara yao tuliyokubaliana na Watakaguliwa na Kampuni za kimataifa zinazoaminika.

Waafrika kiasili si Wanufaishaji wa wengine,na ni limbukeni wa mali,uchoyo na tamaa ya kila mmoja kumzidi Mwenzake ndio tunaona ni maisha.Angalia hata Weusi wenzetu nje ya Africa,Haiti au Jamaica tatizo ni hilo hilo.

Nchi zinatengeneza "untouchables" wanakuwa na nguvu kiasi kwamba walio wengi wanabaki kusubiri huruma ya Viongozi ili hali tuna rasilimali lukuki.
 
Sijaona tofauti hiyo na ukoloni
 
Sijaona tofauti hiyo na ukoloni
Kama unaona hivyo basi tufanye ni aina moja wapo ya ukoloni kati ya aina kadhaa zilizopo,ila ni aina bora kati ya hizo nyingine.

Ingawa mimi ninachomaanisha ni kuwa huyu Manager hatokuwa anawakilisha Nchi yake anayotokea,na atatoka kokote hata kama ni Mtanzania Mwenzetu atakayekidhi vigezo.

Lengo hapa ni kukwepa "Watawala wanaotula wenzao".Kupata madaraka Africa ni njia ya mkato ya kuwa Bilionea na Mmiliki wa rasilimali zote,na haipaswi kwa hivyo.

Manager atasimamia rasilimali za Wananchi wote.

Muda si mrefu hapa Uganda wanaingia kwenye uchaguzi ambao Museveni atashinda kwa kishindo na yatatumika mamilioni ya pesa bila sababu.
 
Back
Top Bottom