Africa as we know it!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Africa as we know it!!

Discussion in 'International Forum' started by Nyodo1, Mar 10, 2011.

 1. Nyodo1

  Nyodo1 Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Things like this happens only in Africa....
  Wakazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam jana walikumbwa na hofu na kusababisha wengine kulazimika kuzikimbia nyumba zao kwa muda, baada ya simba kuvamia eneo hilo na kuwashambulia baadhi yao.
  Katika tafrani hiyo, mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Baba Zai (40), alijeruhiwa vibaya maeneo mbalimbali ya mwili wake baada ya Simba huyo kumshambulia na amelazwa katika Hoapitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.
  Mtu huyo alijeruhiwa vibaya na simba huyo kooni, ambako kwa kawaida mnyama huyo hupendelea kuanza kushika kwa ajili ya kuua kwa urahisi.
  Walioshuhudia tukio hilo walisema lilitokea jana majira ya saa 12: 45 asubuhi katika eneo la Mbagala Kimbangulile, ambapo kuonekana kwa simba huyo kulisababisha watu kujifungia ndani na wengine kuhama nyumba zao kuhofia usalama wa maisha yao.
  Omari Ramadahani (24), alisema tukio la kuonekana kwa simba huyo ilitolewa na jirani yao ambaye alimuona simba akipita nje ya nyumba yake wakati akijiandaa kwenda kazini.
  Alisema baada ya kumuona simba aliamua kuwataarifu majirani zake na ndipo watu wengi walijitokeza na kuamua kufuatilia nyayo za simba huyo ili kujua mahali alipoelekea.
  Omar, alisema katika kufuatilia nyayo, waligundua kuwa simba huyo ameingia katika nyumba moja ambayo ujenzi wake haijakamilika na kujihifadhi.
  "Baada ya kubaini alikojificha, watu walianza kutupa mawe ndani ya ile nyumba, simba aligundua yuko hatarini ndipo alipoanza kuunguruma kwa sauti kubwa na kusababisha watu kupatwa na hofu," alisema.
  Alisema, wakati wanafanya mpango wa kuwasiliana na polisi, jirani yao ambaye alijeruhiwa, alipita karibu na nyumba hiyo akiwahi kazini kwake bila kufahamu kuwepo kwa simba huyo.
  Alipokuwa akipita eneo hilo, ghafla simba huyo aliruka na kumparua kwa makucha mabegani kisha kumuangusha chini na kuanza kumung'ata kwa meno kichwani na sehemu ya kooni.
  "Yule simba alikuwa na nia ya kumtafuna, lakini kutokana na kelele za watu na vurugu za watu kukimbia kunusuru maisha, alimuacha na kuanza kukimbia hovyo mitaani akitafuta mahali pa kujificha," alisema.
  Majeruhi huyo alichukuliwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Temeke na baadaye kuhamishiwa Muhimbili ambako anaendelea kupatiwa matibabu na inaelezwa hali yake ni mbaya.
  Juhudi za kumsaka simba huyo kwa ajili ya kumuua zilizaa matunda majira ya saa 2:00 asubuhi baada ya askari wa Kikosi cha Wanyamapori wakishirikiana na Polisi kumpiga risasi.
  Iliwabidi polisi wafanye kazi ya ziada kumchukua simba huyo kumpeleka ofisi za Maliasili zilizopo eneo la Keko baada ya wakazi hao kutaka kumkatakata ili wagawane nyama yake kwa kuifanya kituweo.
  Alipotafutwa kuelezea tukio hilo, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Devid Misime hakupatikana.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...