Afisa wa Marekani aomba msamaha kwa Libya

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956
10/03/2010

PJ CrowleyAfisa wa Marekani ameomba msamaha kwa matamshi aliyotoa na kuonekana kuwa ni shambulizi kwa kiongozi wa Libya Muamar Gadhafi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje P.J.Crowley anasema matamshi yake kuhusu Bw.Gadhafi kutaka kuwepo kwa jihad au vita vitakatifu, dhidi ya Uswizi haiashirii sera ya Marekani na wala haikuwa na azma ya kuleta ubishani.

Crowley anasema anasikitika kwamba matamshi yake yamekuwa ni kikwazo kwa uhusiano wa Marekani na Libya.

Anasema waziri mdogo wa mambo ya nje Jeffrey Feltman atakwenda Tripoli wiki ijayo kwa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.
http://www.voanews.com/swahili/2010-03-10-voa1.cfm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…